Menu
 

Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Bi Victoria Mbulike Nkopa(42) mkazi wa Airport, Kata ya Iyela, Jijini Mbeya amedai kudhulumiwa mirathi ya marehemu mumewe Gilbert Kapogo, aliyekuwa mwalimu wa Shule ya msingi Mbimba, Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya.

Marehemu alifariki mwaka 2008 na mirathi iliandikishwa mwaka 2009, ikihusisha watoto wawili Joseph Gilbert (12) na Sharida Gilbert(9)ambao wote ni wanafunzi wa shule ya msingi na Mama yao mzazi Bi Victoria.

Kila mtoto katika mgao huo wa mirathi alitakiwa kupata shilingi milioni 8,700,000 kila mmoja, lakini cha ajabu kaka wa marehemu aitwaye Stephano Mbimba mkazi wa Tukuyu Bagamoyo ameweza kutoa mirathi ya mtoto mmoja tu na ameendelea kuhodhi mirathi ya mtoto wa pili bila sababu za msingi.

Msimamizi wa mirathi hiyo Tunsajepo Kapogo amesema kuwa amefuatilia mirathi hiyo kwa muda mrefu bila mafanikio, hali inayopelekea kutaka kujitoa kuwa msimamizi wa mirathi hiyo, kutokana na usumbufu aliouonesha Bwana Stephano.

Hata hivyo watoto wamelazimika kusimama kuendelea na masomo baada ya kuibiwa nguo na vifaa vingine vya shule.

 

Post a Comment

 
Top