Menu
 


Habari na Ezekiel Kamanga, Kyela.
Mwanafunzi wa Kidato cha Kwanza katika Shule ya Sekondari Ikolo, Wilaya ya Kyela Bakiro Hance (18), amekutwa akifanya mapenzi na ng’ombe wa jirani yake.

Tukio hilo limetokea Machi 28 mwaka huu majira ya saa sita mchana katika Kijiji cha Ikolo ambapo mtuhumiwa alimchukua ng’ombe mmoja kati ya wawili wanaomilikiwa na Bwana Dickson Mwakimi, waliokuwa wamefungwa karibu na nyumba anayoishi  mmiliki huyo.

Bwana Mwakimi alisikia ng’ombe wake akitoa sauti isiyo ya kawaida, kisha akatoka nje na kumkuta mwanafunzi huyo akifanya mapenzi na ng’ombe, ambapo alimkamata mwanafunzi huyo alimpeleka kwa mzazi wake aitwaye Bwana Hance, na mwanafunzi huyo alikiri kutenda kosa hilo ingawa hakuweza kueleza sababu zilizompelekea kufanya kitendo hicho cha aina yake.

Ameongeza kuwa mara kadhaa amekuwa akitenda tendo hilo na kwamba alijaribu kumkamata ng’ombe wa kwanza lakini alikuwa mkali hali iliyopelekea kushindwa kutimiza azma yake mwingine wa Bwana Mwakimi, ndipo alipoamua kumkamata ng’ombe wa pili na kumfunga kamba kwenye mti uliokaribu na kisha kuanza kufanya naye mapenzi.

Hata hivyo familia zote mbili za mmiliki wang’ombe na mwanafunzi zinaendelea kufanya mazungumzo ili kuondoa tofauti zilizojitokeza za tukio hilo la ajabu lililofanywa na mwanafunzi huyo.

Post a Comment

Yasinta Ngonyani said... 25 April 2012 at 17:36

Inasikitisha kweli na kama mzazi nimeumia sana. Naomba wazi tuwape elimu za ngono wanetu kwani wazazi ni walimu wa kwanza!!

Chimbuko Letu said... 27 April 2012 at 03:47

Ki ukweli dada siku hizi ni tofauti na zama za kale, fikiria hii leo mzazi ni adui wa mtoto wake hampi ushauri wowote juu ya maisha, na walimu ndo kabisa hawana hata mpango wa kutoa elimu ya waisha kwa wanafunzi wao

 
Top