Menu
 

*Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Mwanamke mmoja aitwaye Ashura Rashid (28), mkulima na mkazi wa Lupa, Wilaya ya Chunya, Mkoani Mbeya amefariki baada ya kuuawa na mumewe kwa kuchomwa kisu sehemu mbalimbali za mwili wake kichwani, mgongoni na mkono wa kushoto.

Mkasa huo umetokea Aprili 9 mwaka huu majira ya saa 10:30 jioni eneo la Kibaoni wilayani humo, huku mumewe aliyefahamika kwa jina la Levocatus Ernest (25) kutoroka mara baada ya kutenda kosa hilo la mauaji.

Chanzo cha mauaji hayo ni mzozo mkali uliozuka nyumbani hapo baina yao hali iliyompelekea mtuhumiwa kuchukua kisu na kuanza kumshambulia marehemu mkewe hadi kumsababishia kifo papo hapo.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani hapa Barakiel Masaki, amethibitiosha kutokea kwa tukio hilo na kwamba Jeshi lake linafanya jitihada za kuhakikisha linamtafuta Levocatus Ernest, ili kumfikisha mikononi mwa sheria.

Hata hivyo amesema kuwa upelelezi wa tukio hili unaendelea, lakini kumekuwa na matukio mengi hivi karibuni mkoani Mbeya ya wanawake kuuawa, chanzo kikubwa kikiwa ni wivu wa kimapenzi jambo ambalo linapaswa kukemewa kwa nguvu zote.

Post a Comment

 
Top