Menu
 


Habari na Mwandishi wetu
Idadi ya wafanyabiashara katika stendi ya mabasi yaendayo Dar es salaam imekuwa ikiongezeka kila siku, hali inayohatarisha usalama kwa wafanyabiashara wa eneo hilo kutokana na wao kufanya biashara zao kando kando ya barabara.

Wakiongea na Bomba Fm wafanyabiashara wa ndizi, viazi na matunda wametoa ombi kwa uongozi wa halmashauri ya jiji kujenga upya kituo hicho cha mabasi ili kuwawezesha kufanya shughuli zao katika hali ya usalama.

Mmoja wa wafanyabiashara hao ATUGANILE MWASAPILE amesema bidhaa nyingi huuzwa eneo hilo jambo ambalo linahatarisha hali ya usalama kwa wafanyabiashara na wasafiri.

Hata hivyo hatukufanikiwa kuongea na mwenyekiti wa soko hilo dogo kwa sababu wafanyabiashara hao hawana mtu anayewasimamia ikiwa ni pamoja na biashara kufanywa katika eneo lisilo rasmi.

Post a Comment

 
Top