Menu
 


Habari na Angelica Sullusi, Mbeya
Serikali imeombwa kutoa taarifa sahihi na kwa wakati muafaka kwa watu wenye ulemavu hususani watoto juu ya mambo muhimu yatokeayo nchini ili kundi hili liweze kushiriki kikamilfu katika masuala mbalimbali muhimu kwa nchi.

Wito huo umetolewa leo na Mshauri wa masuala ya kisheria wa mradi wa watoto wenye ulemavu(YDCP) ulioko chini ya Free Pentecostal Church of Tanzania(FPCT), Gidion  Mandesi wakati akipokuwa akitoa mada katika kikao cha uchaguzi wa viongozi wa baraza la watoto wenye ulemavu mkoani hapa.

Mandesi amesema kuwa kutokuwepo na taaarifa sahihi kwa kundi la watu wenye ulemavu mfano wasioona na viziwi na wakati mwingine kufika kwa kuchelewa kunawanyima haki ya kushiriki katika mijadala mbalimbali ambayo inawahusu.

Ametoa mfano juu ya mchakato wa uundwaji wa katiba mpya pamoja na zoezi zima la hesabu ya idadi ya watu(sensa) ambalo linatarajiwa kufanyika nchi nzima mapema oktoba mwaka huu,na kusema kuwa ni wajibu wa serikali kuhakikisha makundi haya yanapata taarifa sahihi na kwa wakati.

Awali, akizungumzia juu ya haki za watoto Mandesi amesema kuwa watoto wote wanahaki sawa isipokuwa watoto wenye ulemavu hukosa haki hizo kutokana na mtazamo hasi wa jamii inayowazunguka.

Aidha,ameiomba serikali kupitia tume iliyoteuliwa kuhakikisha inapokwenda kukusanya maoni kwa wananchi kutokusahau makundi haya kamwe, kwani watu hawa wana mawazo mazuri ya uboreshaji wa maeneo yanayowahusu.

Post a Comment

 
Top