Menu
 

Jamani yaani sipendi kuandika makala siju article ndeefu ila leo naona nitaandika sana leo au labda kidogo tu ila ai hevu tu.....

Kuna hili suala la Watanzania na kuongea kiingereza hili, limekua ni tatizo linalojirudia kila mara jamani, sasa mimi kama mimi naomba kuuliza swala la Watanzania kutokuongea ngeli vizuri nani alaumiwe?? maana tumeona wanaoshindwa kuongea kiingereza sahihi sio tu wale ambao hawajasoma bali hata walioenda shule bado ngeli inapiga ugoko; na watu wengine tumekua kipaumbeeele kwacheka wachapiaji hao, je ni mfumo wetu wa shule, na vyuo ndio m-bovu? mbona watoto wetu wa siku hizi wanaosoma intanetionali shooli (International school) wanaongea vizuri tu hata yule wa vidudu?? Ina maana kukosa hizi International au watoto kutoka kwenda nchi za jirani kusoma Tanzania tungeendelea kutia aibu milele?


Na je kuna umuhimu gani mtu asome hadi chuo halafu bado hawezi kujieleza hata kwa sentence moja ilioyoonyooka ka kithungu? Je masomo huko chuo yanafundishwa kiswahili au kiingereza? sasa kwanini mpaka tunamaliza chuo English bado inakua no sevisi avoilabo? jamani mweeh..


Kuna huyu mama Rose Daudi Mwalusamba aliejitoa kugombea E.A.C sijui nini nini huko mi sio pabliki politiko sayansi siju,i hata hio E.A.C ndio nini..? nipo hapa kudiskasi vitu vingene.... anyway  nimeona watu wakimjadiiiliii na kumcheeeka na mimi pia nimecheka nilipoisikia hio clip ambayo inazagaa fezibukuni, ila nilipocheka sio kwa kua najua sana ngeli....!! lah hasha....nimecheka kwakua imesound fani, na pia wale wenyewe wanaomrekebisha noa bila bila  sasa wanamchekea nini mama wa watu..!!?? 


Well, siko hapa kumtetea au kukandia mtu ila nauliza tu, hii tabia ya kulazimishana watu kuongea ngeli bungeni imeanza lini? au ni kwamba mama wa watu aliamua tu mwenyewe kuonyesha msisitizo wa hapa na pale?? maana naona isingekua lazima jamani kwenye bunge letu la Tanzania ambapo robo tatu ya nchi wanaongea kiswahili mkawashurutishe watu kuongea kiingereza jamani ...uuwwwiiii wabongo mna mambo nyie....!!?? haya hio I am marriedi with tree crids ndio nini? hehehehehe uuwwwiiiii na my deili bledi ndio nini uuwwiiiii jamani jamani mweeh..!!!??


Ngoja niwawekee link msikilize wenyewe muone kama hii ni haki kwa kuongea ngeli ya kulazimisha, au niongee kiswahili changu nitakachokua komfotabo na kitu ninachosema. 


Ila twende mbele turudi nyuma LAWAMA zoote zielekezwe katika uongozi wa nchi na system ya shule zetu kuanzia za msingi, sekondari mpaka chuo yaani kama baba yako hana uwezo wa kukupeleka intanetionali au nje ya nchi wewe utaongea mai delili bledi mpaka kufa, hehehehe sicheki ila nasikitika sana, yaani kuna ugumu gani wa kuweka msisitizo na kuboresha mfumo mzima wa kufundisha ngeli kuanzia ngazi za chini a.k.a elimu ya awali? kama  hamuwezi kufanya hivyo msilazimishe basi watu kuongea ngeli, kazi kutiana AIBU tuu..


Profeshenari I'm a politician I have a knowledge known as political science, pablik administration and INTERNATIONAL RELATIONSHIP! lol nimeikopi toka kwa mdau mmoja huko fb kama alivyoisikia toka kwa huyo mbunge, kwa msisitizo zaidi click link below


written by

Tina Ndonde

Post a Comment

 
Top