Menu
 

Na Abou Shatry

Timu ya Tanzania DMV imekamilisha madhumuni na malengo ya kuingia rasmi na ligi ya Diaspora World Cup 2012 itakayofanyika Germantown na Hyattsville Maryland, mwanzoni mwa mwenzi huu wa May chini ya mdhamini wa timu hiyo Abdallah wa Vizion One.

Tarifa kwa wachezaji wote mnaombwa kuzingatia mda wa mazowezi mliopangiwa ili kuwa makini na malengo yaliokusudiwa ya ligi ya Diaspora World cup 2012 itakayofanyika Germantown na Hyattsville Maryland,

Pia katika bahati hii ya kushiriki kwenye ligi ya Diaspora World Cup, na kufanikisha malengo yaliokusudiwa, timu hiyo ya TZDMV inawaomba Watanzania wote ushirikiano wenu wa kila hali ili kuipa changamoto timu ya Watanzania DMV pamoja na wachezaji, katika burudani inayopendwa na wengi ulimwenguni, karibuni karibuni sana siku ya sherehe za ufunguzi April 28th ndani ya Discovery Stadium uliopo Germantown SoccerPlex. Stadium.

Milango inatunguliwa 12:00pm, ambapo jamii zote zitawasili kuunga mkono time zao zilizoingia katika ligi hiyo kitaifa kama Diaspora World Cup pamoja na ngoma za kiasili, nyote mnakaribishwa.

Vile vile Vigogo wengi wamethibitisha uwepo wao ikiwa ni pamoja na HE Eklil Hakimi, Mheshimiwa Balozi wa Afghanistan katika Umoja wa Mataifa, HE Joseph Foe-Atangana, Mheshimiwa Balozi wa Cameroon katika Umoja wa Mataifa, HE Perezi K. Kamunanwire, Mheshimiwa Balozi wa Uganda nchini Marekani, HE Adebowale mimi. Adefuye, Mheshimiwa Balozi wa Nigeria nchini Marekani, HE Devinda R. Subasinghe, aliyekuwa Balozi wa Sri Lanka, Waziri Johnny Moloto, Mkuu wa Mission wa Afrika Kusini nchini Marekani, Jenerali Emmanuel Maganga, wa Tanzania katika Ubalozi wa Marekani, na kamanda Luther Reynolds, Mkuu wa Polisi wa Germantown atakuwepo.
Adress MD. 14501 Schaeffer Rd Germantown, MD20874

Post a Comment

 
Top