Menu
 

Mzee Alex Mwang’onda (60) mkazi wa mtaa wa Wakulima eneo la Makunguru ameuawa kwa kuchomwa moto na wananchi wanaojiita wenye hasira kali baada ya kukutwa akiwanga nyumbani kwa Jubel Mbekule, mtaa wa Mkombozi maarufu kwa jina la Kwa Chaula, Aprili 11majira ya saa 10:30 alfajiri.
Mke wa marehemu Bi Amina Alex (42), akiwasihi wananchi wasimpige mumewe hata hivyo wananchi hao walikaidi ombi hilo na walimtembeza utupu Mzee huyo hadi nyumbani kwake amakoishi majira ya saa moja asubuhi na kisha kuanza kumpiga na hatimaye kumchoma moto.
Mke wa marehemu akijaribu kumsitili mumewe kwa nguo, baada ya wananchi kumvua nguo mumewe.
Aprili 11 mwaka huu ambapo Mzee Alex alikutwa akiwa na hirizi mbili, mizizi inayodaiwa kuwa ni dawa ya kienyeji na pesa taslimu shilingi 2, 000 za kitanzania.
Mwenyekiti wa mtaa wa Mkombozi Bwana Alfred Mwasumbi akiwepo eneo la tukio ambaye alishindwa kuwazuia wananchi wamsimtendee ukatili Mzee Alex.
Pichani ni nyumba inayodaiwa kuwa marehemu Mzee Alex alikutwa akiwanga.
Pichani ni gari la Jeshi la Polisi mkoani Mbeya likifika eneo la tukio kwa kuchelewa ambapo walikuta wananchi wamejichukulia sheria mkononi kwa kumchoma moto.(Picha zote na Ezekiel Kamanga).

HITIMISHO:- Wimbi la mauaji Mkoani Mbeya lazidi kupamba moto, Alex Mwang’onda mkazi wa mtaa wa Wakulima eneo la Makunguru ameuawa na wananchi wenye hasira kali baada ya kukutwa akiwanga nyumbani kwa Jubel Mbekule, mtaa wa Mkombozi maarufu kwa jina la Kwa Chaula.<<< Soma zaidi hapa>>>

Post a Comment

 
Top