Menu
 


Habari na Mwandishi wetu.
Wakazi wa mtaa wa Ihanda mji mdogo wa Tunduma wilayani Momba mkoani Mbeya wamehimizwa kushiriki katika ulinzi shirikishi ili kuliwezesha eneo lao kuwa sehemu salama ya mali na maisha ya binadamu.

Rai hiyo imetolewa na Afisa mtendaji mtaa wa Ihanda bwana Olandi Cheyo ambaye amesema kuwa matukio ya uharifu yameanza kujitokeza tena kwenye kata yake baada ya wananchi kuacha kushirikiana katika ulinzi.

Aidha amesema ili kukabiliana na matukio hayo haina budi kwa wananchi wote kushirikiana kikamilifu katika suala la ulinzi shirikishi.

Naye mwenyekiti wa mtaa huo Zabron Pesambili amesema mpango wa ulinzi shirikishi utakuwa wa kudumu ili kukabiriana na vitendo vya wizi.

Post a Comment

 
Top