Menu
 


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mizengo Pinda.
********
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Mizengo Pinda amesema kesho atatoa tamko la Serikali juu ya habari za kuwapo mawaziri ambao wamelazimishwa kujiuzulu na wakakubali. 


Pinda alitoa kauli hiyo jana baada ya kuulizwa na waandishi wa habari juu ya msimamo wake kuhusu habari zilizoandikwa na baadhi ya vyombo vya habari jana kuwa mawaziri wanane wamekubali kujiuzulu kwa kuandika barua baada ya kutakiwa kufanya hivyo na wabunge wa CCM. 


Kikao cha wabunge wa CCM kilifanyika Alhamisi na juzi baada ya wenyeviti wa kamati zinazosimamia Serikali katika masuala ya fedha kuwasilisha taarifa zao zilizoibua tuhuma za ubadhirifu mkubwa wa fedha za umma ndani ya Serikali. 


Pinda ambaye juzi usiku alitajwa na Katibu wa Wabunge wa CCM, Jenista Mhagama kuwa angezungumzia kwa kina masuala yaliyojiri ndani ya kikao cha wabunge wa CCM, hakufanya hivyo hali iliyowalazimisha waandishi wa habari kumvizia kabla hajaondoka kwenye Viwanja vya Bunge. 


Tofauti na ahadi ya Mhagama, Pinda alionekana kutokuwa tayari kuzungumzia suala hilo.

Post a Comment

 
Top