Menu
 


Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Watu wasiofahamika na kudhaniwa kuwa ni wezi wamevunja na kuiba pesa taslimu shilingi 289, 500 pamoja na vitu mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 3, katika Kanisa Katoriki Kigango cha Nzovwe, Jijini Mbeya.

Tukio hilo limetokea Aprili 24 mwaka huu majira ya saa mbili usiku ambapo Bwana Peter Mushi, aligundua kuvunjwa kwa kanisa hilo na kuibiwa pesa zilizokuwa ndani pamoja na vipaza sauti vitatu, receiver 2, vitenge doti 15, pasi moja ya umeme na vitu mbalimbali vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 3,265, 000.

Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kwamba mbinu iliyotumika katika uhalifu huo ni kuvunja mlango wa kanisa kisha kuiba.

Hata hivyo upelelezi wa tukio hili unaendelea na hakuna mtu yeyote aliyekamatwa kuhusiana na tukio hili.

Post a Comment

 
Top