Menu
 

Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Wimbi la wizi wa pikipiki limezidi kushamiri Mkoani Mbeya, ambapo tukio la hivi karibuni limetokea Kijiji cha Malonji, Wilaya ya Mbozi baada ya watu wasiofahamika kuvunja nyumba ya Mwalimu wa Shule ya Msingi Mlonji kisha kuiba pikipiki yake.

Tukio hilo limebainishwa na Mwalimu Simon Mwamkama (54) wa shule hiyo, ambaye ni mkazi wa kijiji hicho Aprili 4 mwaka huu majira ya saa 12 kamili.

Amesema watu wasiofahamika walivunja moja ya vyumba vya nyumba yake kisha kuiba pikipiki aina ya Greenshine yenye nambari za usajili T 719 DMD, ambayo inathamani ya shilingi milioni 1,200,000.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba upelelezi wa tukio hili unaendelea na hakuna mtu yeyote aliyekamatwa kuhusika na tukio hilo.

Post a Comment

 
Top