Menu
 

Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Mtu mmoja wa jinsi ya kiume ambaye hakuweza kufahamika mara moja wala makazi yake amefariki dunia baada ya kugongwa na gari aina ya Toyota Coaster nambari T 715 ATT katika barabara ya Mbeya/Iringa.

Tukio hilo limeyokea Mei 10 mwaka huu eneo la Uyole jijini Mbeya gari hilo likiwa katika mwendokasi lilimgonga marehemu na kumsababishia kifo papo hapo.

Dereva wa gari hiyo amefahamika kwa jina la Bwana Stanley Petro (44) mkazi wa Simike jijini Mbeya.

Kaimu Kamanda wa  Jeshi la Polisi mkoani hapa Barakiel Masaki amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba dereva anashikiliwa kwa uchunguzi zaidi na upelelezi wa tukio hili unaendelea.

Hata hivyo mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa jijini hapa na wito umetolewa kwa yeyote aliyepotelewa na ndugu yake kufika hospitalini hapo kwa ajili ya kuutambua mwili wa marehemu.

Post a Comment

 
Top