Menu
 


Habari na Ezekiel Kamanga, Rungwe.
Mambo juu ya mambo Mkoani Mbeya baada ya Bwana Juma Mwakatabale (30), mkazi wa Kijiji cha Matamba, Kata ya Isange, Wilaya ya Rungwe kufumaniwa na mkewe Bi Emelia Mwakatabale Aprili 29 mwaka huu majira ya saa mbili usiku baada ya kumkuta akifanya mapenzi na mke wa mtu jina limehifadhiwa.

Baada ya wananchi wa Kijiji hicho kupata taarifa ya nyendo zao waliamua kumtafuta Bi Emilia na kuamua kuweka mtego kwa kutumia simu ya kiganjani ambapo alielekezwa na kuamua kuitafuta ndipo ilipotoa sauti ya miito hivyo kuwakurupusha katika tukio (wakira uroda) ndipo BI Emelia aliamua kumrusha chupa ya soda na kumjeruhi kichwani mumewe Bwana Mwakatabale.

Tukio hilo limethibitishwa na Mwenyekiti wa Kijiji hicho Bwana Johani Mwakyoma ambaye amesema wanandoa hao wamesuluhishwa na wameridhiana lakini upande wa pili wanandoa wameamua kutengana.

Hata hivyo kutokana sakata hilo Bi Emelia ameamua kurudi nyumbani kwao kwa madai kuwa kitendo hicho kilichotendwa na  mumewe kimemdhalilishwa kwa kufanya mapenzi juu ya kaburi la baba yake mzazi (mkwe), bila hata kujali kuwa kuna ugonjwa wa UKIMWI kinahatarisha maisha yake.

Post a Comment

 
Top