Menu
 

Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Raia 17 wanaodhaniwa kuwa ni wa Ethiopia wamepata ajali eneo la Stamico, Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya.

Hayo yamebainishwa na Naibu Kamishna wa uhamiaji Mkoa wa Mbeya na Kaimu Afisa uhamiaji wa mkoa Bwana Remigius Ibrahim Pesambili, ambapo amesema ajali hiyo imetokeai Mei 19 majira ya usiku yakihusisha gati nambari T 304 AWF aina aina ya Toyota Hilux ambapo mmiliki wake hajafahamika mpaka sasa na kusababisha vifo vya watu 6 na majeruhi watu 12.

Amesema kuwa maiti 5 za wa Ethiopia hao na mmoja anayedhaniwa kuwa ni mtanzania zimehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa jijini Mbeya, na majeruhi watano wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kyela na watu saba wamelazwa katika Hospitali ya rufaa na kutanjwa afya zao zinaendelea vema.

Kamishna Pesambili amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi na dereva kushindwa kulimudu gari hilo na baadae kusababisha ajali na kikosi chake kunafanya upelelezi kuhusiana na tukio hili.

Hata hivyo hii ni ajali ya pili mfululizo kutokea mkoani Mbeya ambapo ajali nyingine ilitokea Kijiji cha Luswiswi katika Wilaya ya Ileje na kusababisha vifo vya wa Ehtiopia na wasomari na majeruhi kadhaa.

Wimbi la uhamiaji mkoani hapa limezidi kwa kasi kwa siku za hivi karibuni, hali inayodhaniwa kuwepo kwa mtandao wa usafirishaji wa raia hao wa kigeni na kuelekea kusini mwa Afrika kwa kupitia njia za panya, hali inayohatarisha usalama wa nchi yetu.

Post a Comment

 
Top