Menu
 

Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Edward Arabi Mwakilasa (50-55), amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia shuka ndani ya choo cha nyumba yake.

Tukio hilo limetokea Jijini Mbeya, Mtaa wa RRM Mei 5 mwaka huu majira ya saa 8 mchana.

Marehemu alikuwa anaishi na wanawe wawili kabla ya kutengana na Mkewe Bi Kisa Mwakabana kwa zaidi ya miaka miwili.

Marehemu alikuwa dereva tax eneo la Uhindini jijini hapa, ambapo hivi karibuni ilidaiwa amepata ajali na gari alilokuwa akiliendesha.

Aidha siku ya tukio marehemu alionekana mwenye mawazo na baadae hakuonekana hadi pale mwili ulipogunduliwa na wanawe na kutoa taarifa kwa kaka wa marehemu Bwana John Arabi, ambaye alifika nyumbani hapo.

Kaka huyo wa marehemu alitoa taarifa katika Kituo cha Polisi cha Kati, ambapo walifika na kuuchukua mwili wa marehemu hadi Hospitali ya Rufaa iliyopo jijini hapa kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Hata hivyo hakuna ujumbe wowote ulioachwa na marehemu juu ya kifo chake na Jeshi la polisi linafanya uchunguzi kuhusiana na kifo hiki.

Post a Comment

 
Top