Menu
 

Wakati mashabiki wa Big Brother Afrika wakisubiri kwa hamu uzinduzi wake msimu huu wa saba Jumapili hii, majina ya washiriki wa Tanzania bado ni kitendawili. 

Tayari washiriki saba kutoka Kenya, Namibia, Zambia, Afrika Kusini na Nigeria wameshajulikana lakini kwa Tanzania bado majina yanasubiriwa kwa hamu kama linavyosubiriwa baraza jipya la mawaziri! 

Kila mmoja anasema yake, lakini siku za hivi karibuni Jokate Mwengelo anatajwa sana kuwa ni miongoni mwa washiriki wawili watakaowakisha Tanzania. Lakini swali ni kuwa, atawezaje kuwakilisha Big Brother wakati tayari ni mwajiriwa Channel/DSTV ambao ndio wamiliki wa reality show hiyo?

Maswali mengi katika mtandao wa twitter yameelekezwa kwake na watu ambao wanataka kujua kama yeye ndiye atakuwa mwakilishi mmoja kati ya wawili kutoka Tanzania!

"Mna yenu, mi niko hapa kama rep wa Channel O tu! aliandika Jokate.

Post a Comment

 
Top