Menu
 

Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Ayoub Mwamboma mkazi wa Sinza, Wilaya ya Chunya, Mkoani Mbeya amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia kamba aina ya manila nje ya nyumba ya mjomba wake mita chache kutoka nyumbani kwake.

Marehemu alikuwa muuza  vinywaji baridi katika Depot ya Bwana Nestory Ndelwa, ambaye ni wakala wa Kampuni ya Cocacola ambapo alidaiwa kuhusika na upotevu wa pesa za mwajiri wake.

Mei 6 mwaka huu mwajiri huyo alikuwa na kikao na marehemu pamoja na ndugu zake na kudai ameingia hasara ya shilingi 2,000,000 hali ambayo marehemu alikanusha na kwamba mwajiri alimtaka kulipa shilingi 50,000 kila mwezi jambo ambalo alilikataa.

Mara baada ya kikao hicho Bwana Ndelwa alimwambia kuwa marehemu atampeleka Polisi Mei 7 mwaka huu ili amfikishe mahakamani.

Uchunguzi umebaini baada ya kauli hiyo na kikao kumalizika marehemu alighadhabika na kuchukua jukumu la kujinyonga kwenye mti uliopo nje ya nyumba ya mjomba wake Bwana Leonard Mwamboma, kutokana na baadhi ya watu aliowakopesha kreti zaidi ya 131 kukataa kumlipa(jina limehifadhiwa) na kwamba baada ya kushawishiwa mudaiwa alidai angelipa kreti 35 mei 7 .

Aidha Polisi walifika eneo la tukio kwa kuchelewa kutokana na kutumia muda wa masaa 4 kwa kilometa 50 licha ya kupewa taarifa toka saa 12 asubuhi na kuuchukua mwili wa marehemu kwa ajili ya uchunguzi na mara baada ya kukamilika mwili ulikabidhiwa kwa ndugu zake kwa ajili ya kuufanyia mazishi katika makaburi ya Kibaoni wilayani humo.

Hata hivyo katika uhai wake marehemu ameshawahi kuwa mchezaji wa mpira wa miguu kupitia timu ya Itewe City na Leopard zote za Wilaya ya Chunya kwa nyakati tofauti.

Post a Comment

 
Top