Menu
 


Wakati Teclar anapewa taarifa ya kuwa ameondolewa kwenye jumba la BigBrother, Julio aliyekuwa amevaa miwani meusi hakuonekana kuwa na wasiwasi wowote. Hilda aliyekuwa ameishika bendera ya Tanzania, wasiwasi ulikuwa umemjaa kama kifaranga kilichomuona mwewe.

Alionekana ameshika mdomo kwa butwaa baada ya Teclar kutangwazwa kufungasha vilago. Kwa pozi mtangazaji IK wa Nigeria akamtangaza Julio kuwa naye anafungasha vilago.

Hilda akamkumbatia Julio kwa simanzi zito. Hilda wasiwasi ukaongezeka. Tofauti na walivyotegemea wengi. Hilda naye akapewa habari mbaya kuwa bata za siku saba mjengoni zinaishia hapo.

Machozi yakamtoka lakini kwa ujasiri akaichukua na kuizungusha bendera ya Tanzania huku umati uliokuwa ukishuhudia tukio hilo ukimshangalia. Na huo ndo umekuwa mwisho wa Tanzania katika msimu huu wa Big Brother Afrika.

Kutangazwa kwa wawakilishi wa mwaka huu kutoka Tanzania katika mashindano hayo haukuwashtua wengi. Huenda hiyo ikawa ndio sababu namba moja ya kwanini watanzania hawakushawishika ipasavyo kuwapigia kura washiriki hao ili kuwaokoa baada ya kutajwa kuwa hatarini kuondoka kwa mara ya kwanza.

“People are not voting na bado mnalalamika.. Ndio tujifunze” iliandikwa kwenye page maalum ya Twitter ya BBATanzania.

Siku chache zilizopita kulikuwa na kampeni nzito ikiendelea kwenye mitandao ya kijamii kuwasisitiza watu wawaokoe washiriki hao. Baada ya kutolewa kwa Julio na Hilda, Twitter iliyokuwa imetawaliwa na mambo yanayohusu Big Brother ikapoa kama maji ya mtunguni. Wazungumzaji wazuri wa BBA wakajifanya hawajui kilichotokea. Mada zikawa ni kuhusu Kaseja kukosa penalty na Machenster United kuichapa Sunderland.

Angalau Hamis Mwinjuma ‏ @MwanaFA alikuwa na la kusema “siku 'nzuri' sana hii..United + Simba + BBA...niice..Biggie angemtoa na Prezzo kabisa ili kesho wiki ianze with no strings attached...” (Kwa hisani ya eotainment.blogspot.com)

Post a Comment

 
Top