Menu
 

 Kutana na kijana Erick Adam Masia si unajua yeye ndiye ameigiza kwenye tangazo la balo.

Season 6:- 
 Kwakua aliondoka mule bafuni kwa hasira alikuwa anatembea bila uangalifu jambo lililomsababishia kukatwa na kioo kilichomdondokea kutoka kilipokuwa kimewekwa dirishani pale kwenye korido alipokatiza na mahasira yake, eti hadi muda huo sijajua sauti yake nkabaki tu namshangaa nakujiuliza huyu ni bubu au vipi? "Ballo umemfanya nini ma mdogo?" ilikuwa ni sauti ya Joy baada ya kurudi na Jesca kutoka dukani kuninunulia nguo...
 "jamani ma mdogo jamaaaani kwani imekuwaje tena jaman Ballo umemfanyaje?" alilalamika Jesca huku akimnyanyua pale chini akisaidiana na Joy... "wala sio ballo ni yeye mwenyewe dada ameumia!" alinitetea binti wa kazi akitokea ndani na pamba na kichupa kidogo nadhani ni cha dawa... "kwani ilikuwaje?" aliuliza Joy huku akimwachia ma mdogo wake akae kwenye kochi... "Sikia dada huyu Ballo alipokuwa bafuni ma mdogo alimfata na mimi nkaenda kumtoa sasa eti ndio kachukia akatoka kwa hasira akakigusa hicho kioo hapo kwa bahati mbaya ndio kikamkata!" alitoa maelezo hayo binti wakazi...
 "Eeh ballo pole mwaya kwa usumbufu msamehe tu ma mdogo wetu ni mgonjwa ana pepo wa ngono huwa inatokea anawakamata hadi machinga wanaotembeza urembo!" alielezea joy wakati huo jesca alikuwa anaendelea kumsafisha lile jeraha... "Huduma zao hapa ni nzuri sana yaani" alisema Jesca wakati tukiwa tunaingia kwenye tax baada ya kuhudumiwa pale Marie stopers... "sasa jesca si itabidi tumpeleke Ballo hadi kwake jaman?" alisema joy na wote tukaongozana hadi sinza mori ninapoishi, nilishuka kwenye tax na kuwapa mshtuko baadhi ya majirani walioniona asubuhi nkiwa mzima halafu muda huo wananiona nimebandikwa maplasta kibao... 
"Pole kaka sijui umefanyaje tena ukaumiaa hivyo?" aliuliza dada bonge mwenye duka jirani kabisa na nyumba ninayoishi... "nimeanguka na pikipiki.." nilijikuta namdanganya japokuwa sikujua kwanini nimedanganya na kuingia ndani kupumzika... "hodii! Hodii! Hoooooddiiiiii..." ilikuwa ni sauti nyororo ya mtoto wa mwenye nyumba ya jirani aliyeja pale eti kunipa pole tu halafu eti amevaa kanga moja tu...
"ahsante dadangu" nilimjibu yule dada... "kaka mbona hunifungulii mlango? Au hutaki niingie ndani kwako?" alisema yule dada na kuingia ndani baada ya kumfungulia.... Je unajua nini kinaendelea?

Post a Comment

 
Top