Menu
 

Kwanza naomba nitambue  uwepo wenu kwa kila dakika ndani ya  ukurasa wa ChingaOne blog! 

Safari yangu  niliyoianza mwaka jana hadi leo hii ni ndefu sana kwangu na ni moja ya hatua kubwa kwenye maisha na mipangilio yangu! imekuwa yenye milima na mabonde, vikwazo na changamoto nyingi  ila nyinyi mnanisaidia mizigo yangu na kufanya safari yangu kuwa nyepesi sana! 

Kuna mengi yanatokea, yakukatisha tamaa yanayonifanyika  nyuma ya masikio na macho yenu ambayo kama binadamu wa kawaida inafikia wakati wa kuona hakuna sababu ya kuendelea ila nyie mmekuwa liwazo langu na kufanya nisonge mbele!

Nimepokea vitisho, maneno ya kashfa , kejeli na mengi yakutia hasira toka kwa baadhi ya watu , Akaunti yangu ya Facebook imejaribiwa mara nyingi  kuharibiwa na kufungwa, kurasa yenu pendwa ya chingaone imepata matatizo ya kimtandao na kutumiwa Virusi ili isiweze kuwa hewani  ila uwepo wenu unanifanya nipigane na kusimama imara ili niweze kuwapa kile kitu mlichozoea!

Muda si mrefu nimepokea meseji nyingi mbaya,  toka kwa mtu mmoja anayetumia jina la Angel Masawe  toka kwenye Mtandao wa Facebook aliyejisajili kama anaishi Tanga - Tanzania . Nia na madhumuni yake inaonyesha wazi kuwa na chuki na ChingaOne blog   bila kuwa na sababu za msingi! na kwa maelezo yake au kwa amri yake angependa ChingaOne blog iache mara moja kuwepo angani na kuendelea kutoa habari! kaahidi kurusha picha zangu kwenye mitandao ya picha za  uchafu  na kunipa baadhi ya anuani ya hizo site kwa lengo la kuharibu taswira yangu machoni kwenu , na hiyo kazi kaahidi kuwa ataifanya muda wowote kuanzia sasa kama sitafanya  anavyotaka yeye!

Nia ya kuandika waraka huu kwenu ni kuwajulisha yote yaliyo nyuma ya pazia na kuwa tahadhalisha kwa lolote mtalolisikia au kuliona kutokana na kauli zake ili lisiwe geni kwenu! kwani binafsi sina mpango wa kusitisha kurusha chochote kama yeye anavyotaka ila nitafanya kama ilivyo ada ya ChingaOne kwa kazi zake za kila siku!

Naendelea kutambua Uwepo wenu katika kurasa yangu, msisahau  kuwa Uwepo wangu ni kwa ajili yenu! Nitaendelea kupambana hadi dakika za  mwisho.

ChingaOne

Post a Comment

 
Top