Menu
 

Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Maiti iliyokuwa imesusiwa na ndugu zake siku nne zilizopita umezikwa kwenye nyumba ya milele jana katika makaburi ya Iwambi jijini Mbeya.

Mazishi hayo yamefanyika baada ya Kituo cha redio Bomba FM cha Mkoani Mbeya, kuendesha harambee kupitia kipindi chake cha Amka Bomba ili kupata fedha zilizosaidia kununua jeneza na baadae kushirikiana na viongozi wa Kijiji cha Nzovwe, ambapo pia kituo cha redio kilitoa usafiri wa kuchukua jeneza hadi Hospitali ya Rufaa.

Baadae kilichukua jukumu la kuutoa mwili wa marehemu kutoka hospitalini hapo hadi makaburini kupitia kijijini hapo ambapo sala fupi ilifanyika ya kuuaga mwili wa marehemu aliyewaacha watoto wanne ambao sasa ni yatima baada ya baba yao pia kufariki 2005.

Mchungaji akizungumza katika neno aliwaasa wananchi kwa kusema hakuna binadamu anayepaswa kumuhukumu binadamu mwenzie bali hukumu ya haki hutolewa na Mungu pekee za kuzitaka pande zote za familia kutokuwa na marumbano tena.

Marehemu alikuwa akiishi mtaa wa Iyela jijini Mbeya na kufariki Mei 7 mwaka huu majira ya saa nene mchana katika nyumba inayomilikiwa na Bwana Giseon Kyebeleka, ambaye ni Askari magereza wa Chuo cha Magereza Kiwira mkoani Mbeya.

Aidha inadaiwa marehemu alifariki kutokana na maumivu ya kichwa kutokana na kupiga nondo hivi eneo la Sido jijini hapa alipokuwa anarejea nyumbani majira ya usiku. (Endelea kutembelea mtandao huu ili kupata picha zaidi za tukio hili)

Post a Comment

 
Top