Menu
 

MADA:- Ajira kwa watoto ambao hutumikishwa katika kazi ngumu za hatari(machimboni, ngono, wizi, ufyatuaji tofali n.k). Je nini kifanyike?
Mtangazaji:- Greyson Salufu Chatanda a.k.a Chris Bee
Muda:- Saa 4:00 usiku mpaka 7:00 usiku.
Kipindi:- Bomba Special Show
Kituo:- Bomba FM Redio 104.0Mhz
Mahali:- Mbeya Tanzania.
<<<Bofya hapa kusikiliza live Bomba FM Radio>>> 
Maoni ya wadau:-
Michael Minja Mimi naona kuwe na sheria zitakazo kuwa zinamlinda mtoto ili asiweze kutumikishwa kinyume na umri wake alio nao. Big up kwa Joshua Turuka, Emmanuel James Nyambo pamoja na Yohana Shombe.

Rais Wa Wastarabu Kwanza kabisa serikali inabidi wafutilie hili suala kwa ukaribu sana maana kumtumikisha mtoto kazi ngumu chini ya miaka 18 ni kosa kisheria wapige marufuku kwa waajiri wote wanaofanya kuwaajiri watoto hawa maana bila hawa wanaowaajiri sidhani kama kungekuwa kuna ajira kama hizi na pamoja kwa kusizia kwa serikali pia kunafanya ajira hizi ziendele kujitokeza

  Simon Marianus Kutoka pale pale dar city niite simon marianus.! Tatizo la watoto kutumikiswa kwenye kazi ngumu hii inatokana na hali ngumu ya maisha, kitu ambacho kinatakiwa kifanyike ni serikali kuweka mipango madhubuti juu ya watoto wa aina hii may be kwa kuwaendeleza ki elimu, maana watoto wote wanaotumikishwa kwa kazi ngumu si kwamba wanapenda bali inabidi wafanye vile ili wa gain kitu
 
Joshua Turuka Hapa nchini sheria za watoto hazitiliwi maanani hivyo ni jukumu la vyombo husika kutendea kazi jambo hili. By Joshua wa MJ..

Beatrice Vedastuce Jamii ielimishwe umuhimu wa maandalizi ya taifa la kesho.nadhani tukielimika hakutakua na malalamiko kama haya.@mic u grey

Eliud Samwel Pia ingekua vizuri kama serikali itaweka sheria ya kimo na umri wa kuajiri watoto hiyo inaweza kusaidia sana kupunguza kero na mateso kwa watoto

Halfa Chimwala Waajiri wachukuliwe hatua kali za kisheria.....Naomba wimbo wa Rama dee"najua" maalum kwa wanafunzi wa cdti uyole.

Alfred Mbwile nakupata live bro toka pande za mwanza. ajira kwa watoto kiukweli sio poa huko kwetu Nonde zipo sana, hai kwa mama yangu akiwa Nonde Mbeya

 King Mengi Meackey Nakupata saaaana hapa Bomba FM unatisha bhana. nipigie ngoma ya jirani ya jitu zima d.Faz imburudishe my love wangu angelina. Coz kila raia wa Tanzania anatambua madhara ya ajira kwa watoto wadogo, basi bora kila mtu ashikilie msimamo pale mwajiri anapopatikana basi sie raia ndo tuwe mstari wa mbele kupinga na kumchukulia hatua tatizo litaisha tu. Wananchi wenyewe sie ni msaada tosha kwa watoto.

   Elifazi Doctorfazi Mtwale leo nipo chuon leo so nakupata bila chenga Grey, funguka na ukurasa mpya!!! LIVE BILA CHENGA JIRANIIIIIIIIIIIIIIIII AYAAAAA
KILA SIKU NATAMANI  ILE KINYAMWEZI YANI GREEEEEEEEEIIIIIIIIIIIY
bwana we serikali iingilie kati Grey maana hilo si jambo jema

Rais Wa Wastarabu Elimu ya ajira kwa watoto kwa waajiri inatakiwa kuwapatia maana mwaajiri kama mwaajiri yeye hajali utu wa mtu ilemladi yeye kazi yake imetendeka basi kwa hiyo anakua hajui madhara ya kuwaajiri watoto

Eliud Samwel Hapo cha msingi kwanza kila raia aweze kutambua thamani na utu wa watoto ili waweze kuisaidia serikali katika kuwaadabisha hao waajiri,kwani mambo hayo yanafanywa uswahili na tunaoshuhudia ni sisi raia wa kawaida lakini matokeo yake tumekua tukikaa kimya bila kutoa taarifa na kuwafichua watu hao

Rehema Benard waajiri wawaone hao kama watoto wao so wasiwafanyishe kazi ngumu kwani wao hawapendi kuwa ivyo ni maisha tu....

Maiko Jacob watoto wanafanyishwa makazi hadi wakomae kwasababu bado hatuna sheria zinazo wakabili mabosi wetu na ndio maana hawachaguwi kuwa huyu ni mtoto au laa. mkuu Greyson Chris Bee Salufu pamoja sana.

Banee Nswila kaka ajira kwa watoto ni unyanyasaji kwa kiwango kikubwa kama vipi wanaowaajili na kuwasurubisha wanatakiwa wapewe adhabu kali ni hayo tu mi nipo moro...mi nipigie nyimbo yoyote ya watu wangu mbeya

Erick Adam Masia Kwa jina naitwa Erick Masia a.k.a 'Ballo' watoto kuajiriwa ni kosa la kisheria na haya yote yanafanyika kwa kukiuka sheria kwahiyo la kufanyika ni kutekeleza sheria zilizotungwa na kuwekwa kwenye kumbukumbu bila kutekelezwa... Inaonikana sisi ni wepesi wa kutunga sheria lkn ni wagumu kuzitumia kuwawajibisha, ni pia sisi wenyewe majirani wa hao watoto wanaotumikishwa tumekuwa wakimya tukiamini kuwa hayatuhusu...

Post a Comment

 
Top