Menu
 

MADA:- Tabia ya baadhi ya wanawake kuwachukua mabinti Vijijini kwa mbinu ya kufanyakazi za ndani (House Girl) na badala yake wakifika Mjini hali inakuwa tofauti na kuwatumikisha mabinti hao katika biashara ya ngono, Je, unadhani inajenga picha gani?
Mtangazaji:- Greyson Salufu Chatanda a.k.a Chris Bee
Muda:- Saa 4:00 usiku mpaka 7:00 usiku.
Kipindi:- Bomba Special Show
Kituo:- Bomba FM Redio 104.0Mhz
Mahali:- Mbeya Tanzania.
<<<Bofya hapa kusikiliza live Bomba FM Radio>>> 
Maoni ya wadau:- 
 Enock Eliud Kihali hiyo si sawa kaka huo ni unyama unaotakiwa kukomeshwa.
Eliud Samwel Kiukweli hilo ni tatizo ambalo kwa sasa limekua ndo kichocheo kikubwa sana katika maambukizi ya virusi vya ukimwi na mimba kwa vibinti vidogo
pia hii inawagalimu maisha yao yote mabinti hao ambao hata elimu ya maambukiz ya VVU hawana.

Msifuni Tweve Wa iringa kiukweli nalaani vikali sana kwa wale wote wenye tabia kama hizo,kiujumla wanaleta picha mbaya sana katika jamii.

KAKA TABIA HII INAJENGA PICHA MBAYA KWA JAMII,NDIYO MAANA AKINA MAMA HAO WANAADHIBIWA NA SHETANI,WANAJIKUTA MAHOUSE GIRL HAO WANAJIKITA KIMAPENZI NA MABWANA ZAO,HII NI LAANA,NAWASII BAADHI YA AKINA MAMA WANAOWAGEUZA MAHOUSE GIRL KUWA BIDHAA ZA UKAHABA WAACHE MARA MOJA, MUNGU HAPENDI BY JOJ SINKOLONGO MBOZI.

WILLY MGALA SHILANGA SISI WAZAZI NDIO TUMEKUwA MSTARI WA MBELE KUWARUHUSU WATOTO WETU WAENDE WAFANYE KAZI NA WATU HAO HUJA KWA MANENO YA ULAGHAI KUMBE NI MATAPELI WILLY MGALA.

Daniel Donald Hawa wanawake wanaofanya hivyo ujue wenyewe wameshakubuhu na miili yao imeshaishiwa masoko sasa kutokana na biashara yao ndio hiyo hawawezi kuiacha ndo maana wanajaribu kutafuta njia m'badala na kiukweli wanawaharibia sana maisha ya hawa mabinti

  Alex MwaLyego hao wanaofanya hivyo wachukuliwe hatua za kisheria pamoja sana ...siku hizi utu hauthaminiki... hapo ni kumwomba tu Mungu apishilie mbali pepo huyo mchafu

Zerah Omary kiukweli haileti picha nzuri na huko ni kukosa utu,sisi binadamu sasa hivi tumekuwa kama wanyama roho zetu mtu yuko tayari kuua ili mradi apate pesa.

Chagga Bouy ebwana hii isue Yup! Its true bravo.
kusema kweli haijakaa njema mkubwa kwani sisi sote ni ndugu, na mtoto wa mwenzako niwako, mtu kama huyu akijulikana anafanya hizi mitikasi inapaswa achukuliwe hatua kali za kisheria.

Michael Minja Hakuna kitu kibaya na chenye dhambi kubwa kama hiki cha kumchukua mtoto wa mtu kwa wazazi wao na kuwaahidi utaweza kumlea kama mwanao. Na kinachokuja kusikitisha zaidi ni kwamba mzazi huyu huyu anakuja kuyasahau yale yote aliokuwa ameyaahidi kumtekelezea mtoto na badala yake anakuja kumshirikisha katika vitendo viovu kiukweli hili sio jambo zuri.


  Emmanuel James Nyambo Ni tamaa ambazo zinawapeleke wanawake hao kuwa na katabia kama hako ni aibu sana sheria ichukue mkondo wake.

Efratechnology Efrachemical Cha ajabu unakuta yeye mwenyewe ana watoto wa kike wenyekuweza kumudu hiyo biashara lakini hata hawauzishi kwa hapo kaka nadhani hawa watu wanakosa kuwa na utu.

Joshua Turuka Haileti picha nzuri kwa kweli watu kama hao wachukuliwe hatua za kisheria ikiwemo kupelekwa ktk vyombo vya haki za binadaamu kama vile Ustawi wa jamii.

Maiko Jacob hakuna kitendo kibaya kama hiki na cha wanaojitokeza kusema nafanyishwa mambo hayo na ndio maana hii tabia bado inaendelea mpaka sasa.

Alex MwaLyego ila naomba tuangalie na upande wa pili...maana kuna watoto wengine wakifika town wao ndo wanasoma alama za town...wanaacha kile kilichowaleta na kujiingza ktk vitendo vya ngono...

Ni Kusahau utu ni nini na kujali pesa. Unajua nini ma brother ukizungumzia ni vitu gani vina run dunia basi lazima utataja pesa na mapenzi, hivi viwili hutegemewa sana. Wanawake huwachukua mabinti tena huwaomba wazazi wa mabinti hao huku wazazi wakiamini mabinti zao wanaenda kutafuta pesa kwa ajili ya nyumbani. Lakini wakija mjini ndio wanajikuta kwenye biashara ya ngono. Wanakuwa hawana la kufanya na kukubaliana na matokeo na inapelekea kukubali kutokana na sababu zifuatazo:-

1, ELIMU- Ni chanzo cha ujinga ambacho binti anapokuja mjini anakutana na watu ambao humlaghai na kumshawishi kuingia kwenye biashara hiyo sasa kutokana kukosa elimu anakuwa hana la kufanya kwa sababu kazidiwa ujanja.

2. MAISHA- Maisha ya kijijini na msoto aliopitia kijijini anaona ni vema akubali kuingia kwenye biashara hiyo maana ameshaambiwa pesa atapata zaidi na akikumbuka home life gumu.

3.UTU- Ubinadamu umetoweka kabisa na ushetani umeingia maana pesa imeshakuwa ndio kila kitu mtu yuko tayari hata kumuuza binadamu mwenzie au kumfanyia kitega uchumi kwa sababu ya pesa so utu umepotea sana.

HITIMISHO/MAONI
Hebu nyie mnaofanya tabia hii jaribuni kuishi kwa kujali ubinadamu na co pesa
ni hayo tu thanks.

Huyo mtu wa tabia hiyo anatakiwa kuchukuliwa za kisheria au kifungo cha miaka mitano ni Njile Joseph nipo Ipwizi Mbeya.

Steve Mwashambwa wa Kanga Mkwajuni mi nafikiri wazazi wa watoto wawewanafika mpaka kule ambako mwanae anaenda kufanya kazi.

KIUKWELI HUO NI UTOVU WA UTU NA KUTOTHAMINI UBINADAM KWA SABABU TUMEUMBIWA UPENDO UJUMBE MAWASILIANO NI MHIMU NA KUTEMBELEA WATOTO WALIKO KAZINI KUNA UMUHIMU SANA BY LUTE FRM RUKWA.

MIMI NAOMBA SHERIA IWEKWE JUU YA WATOTO WANAOFANYISHWA KAZI YA BIASHARA YA NGONI NI AMANI MKONDYA UBARUKU

Post a Comment

 
Top