Menu
 

Habari na Rashid Mkwinda, Mbeya.
Jumla ya miradi  9 yenye thamani ya zaidi ya sh. milioni 291.7 imezinduliwa na kuwekwa mawe ya msingi wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru uliokimbizwa katika wilaya mpya ya Momba mkoani Mbeya.

Mwenge wa Uhuru ambao umemaliza mbio zake katika wilaya ya Chunya na kuanza rasmi mbio zake katika wilaya ya Momba na kujenga historia ya kuwa wilaya ya kwanza mpya kukimbizwa mwenge kati ya wilaya 19 mpya zilizoanzishwa hivi karibuni.

Mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo zimezindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali ya huduma za kijamii ikiwemo elimu, Kilimo, afya,Ujasiriamali,Ushirika na hifadhi ya mazingira.

Akitoa taarifa za miradi hiyo mbele ya kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Kapteni Honest Mwanosa, Kaimu Mkuu wa wilaya ya Momba Bw. Jofrey  Kikosa amesema kuwa kati ya gharama za miradi hiyo jumla ya sh. milioni 17.2 zimetokana na michango ya wananchi  ambapo kiasi cha sh. milioni 166.6 zimetokana na mchango wa serikali kuu.

Aidha Bw. Kikosa amesema kuwa kati ya fedha hizo jumla y ash, 342,000 zimetokana na michango ya wahisani ambapo kiasi  cha sh. zaidi ya sh milioni 91 ni michangi ya watu binafsi huku kiasi cha zaidi ya sh milioni 7 zimetokana na mchango wa halmashauri ya wilaya.

Kwa upandee wake Ofisa Utumishi wa wilaya ya Mbozi Bw. Noeli Abel ambaye amesoma risala ya Mbio za Mwenge kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo alisema kuwa miradi iliyofunguliwa na bio za wenge wa Uhuru ni pamoja na mradi wa Biogas uliopo katika kijiji cha Chole,Ujenzi wa zahanati na ujenzi wa hosteli ya wasichana shule za sekondari Ivuna na Chitete.

Ameitaja miradi mingine kuwa ni pamoja na   ujenzi wa nyumba ya kulala wageni iliyopo kijiji cha Ntungwa, kukagua mradi wa nyuki,ujenzi wa shule ya chekechea Parokia ya Chitete na ujenzi wa nyumba ya mratibu wa elimu Chitete.

Akizungumzia ujumbe wa mwenge wa Uhuru mwaka 2012,kiongozi wa mbio za mwenge Kapt.Mwakanosa amesema kuwa mbio za mwenge mwaka huu zimelenga katika hamasa ya kujitokeza katika sensa  ya watu na makazi Agosti 26 ambayo ni wajibu wa kila mwananchi kujitokeza kuhesabiwa kwa nia ya kuirahisishia serikali mipango yake ya maendeleo kwa watu wake.

Pia Kapteni mwanosa amewataka wananchi kujitokeza kutoa maoni juu ya marekebisho ya Katiba ambayo yataliwekea Taifa mkataba na wananchi wake na serikali  kwa nia ya kuboresha mahitaji muhimu ya kijamii, kisiasa na kiuchumi.

Post a Comment

 
Top