Menu
 

*Watatu wakiri hadharani na kukabithi mikoba yao.
*Wachanjwa chale hadharani na Mganga wa Jadi.
*Watozwa shilingi 400,000 kila mmoja kama adhabu.
 *******
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Watu watatu wanaoshukiwa kuwa ni washirikina wamekiri hadharani katika mkutano wa hadhara, uliofanyika katika Mataa wa Mwambenja, Kata ya Iganzo Jijini Mbeya, mbele ya Mganga wa Jadi Nestory Vitus Kasonso mwenyeji wa Laela, Sumbawanga Mkoa wa Rukwa.

Tukio hilo limetokea Mei 14 mwaka huu majira ya saa 8 mchana baada ya mganga huyo kufanya msako wa kuwabaini wachawi katika mtaa huo baada ya kuombwa na wakati wa mtaa huo, kutokana na kukithiri kwa vitendo vya kishirikina mtaani hapo.

Imedaiwa kuwa baadhi ya wakazi wa mtaa huo wamekuwa hawana maendeleo kutokana na pesa kupotea katika mazingira ya kutatanisha, mifugo kufa na watoto kuanguka mashuleni mara kwa mara hali iliyowafanya kuitisha mkutano huo, ambapo awali aliletwa Mganga wa Jadi kutoka Manienga Wilaya ya Mbarali, Bwana Mzungu Pondanga (49), ambaye alifanya kazi kwa siku kadhaa baada ya kusitishwa mkataba wake.

Sababu za kusitishwa kwa mkataba huo ulitokana na sababu za wananchi zakutaka awabainishe hadharani wale wote wanaojihusisha na vitendo vya kishirikina, ambapo mganga huyo alikataa kwa kile alichodai ni kuhofia uvunjifu wa amani mtaani hapo na wananchi kuona kuwa hawajatendewa haki na hivyo kufanya kazi kwa simu moja tu Aprili 29 mwaka huu ambapo matunguli kadhaa yaliteketezwa kwa moto.

Baadha ya hapo Kamati maalum iliyochaguliwa na wananchi na kupata baraka kutoka kwa Chifu wa kabila la Kisafwa Bwana Ndasya waliamua kumtafuta Mganga mwingine wa Jadi ambaye walimtoa Laela Bwana Kasondo ambaye aliahidi kuwataha wachawi wote na kwamba hakutakuwa na uvunjifu wa amani.

Aidha Bwana Kasonso baada ya kukagua maeneo yote kwa makini kwa majuma mawili tangu Mei mosi ndipo aliitisha mkutano wa hadhara jana na kuwabainisha watu watatu wawili wakiwa wanaume na mmoja mwanamke.

Watu hao waliotanjwa hadharani ni pamoja na Daud Mwakalobo, Inspector Mwanjabala na Bi Upendo Kapinga ambaye ni Mke wa mwilu mmoja jijini hapa.

Katika makubaliano baina ya Kamati ya mtaa na Mganga ilikubaliana yeyote atakaye toa kwa hiari yake matunguli yake atatozwa shilingi 100,000 na ambaye atakutwa na mganga huyo atatozwa shilingi 400,000 kama adhabu.

Kutokana na zoezi hilo wote watatu walikutwa na mganga huyo na kukiri kujihusisha na vitendo vya kishirikina na kwa kudhihirisha hilo walikutwa na pembe za ng'ombe na mifupa ya ndege kama bundina dawa zilizochanganywa nyingine zilikutwa chooni na vyumbani ambazo zililetwa hadharani na kuchomwa.

Baada ya kuchoma moto lilifuata zoezi la kuchanjwa chale na mganga ambapo wote wawili (wanaume), walichanjwa hadharani sehemu mbalimbali za miili yao kama kichwani (utosini) na paji la uso miguuni, mikononi na maungoni huku mganga huyo akiwashindilia dawa nyeusi iliyosagwa mithili ya unga laini na kupewa sharti la kutooga kwa siku moja.

Aidha yalitokea mabishano makali baada ya Inspector Mwanjabala kujaribu kukataa kuchanjwa chale ndipo mkutano ulipiga yowe la kumtaka ahame mara moja ndipo alikubali na kuchanjwa bila ubishi.

Bi Upendo Kapinga alienda kuchanjwa katika nyumba jirani ili kumstahi kutokana na makubaliano ili kutunza utu wa mwanamke ingawa zogo lilitokea ikidaiwa naye achanjwe hadharani ambapo wengine walikejeri ku wa mbona wengine humwaga hadharani huku wakiwa utupu.

Baada ya zoezi hilo mganga aliwaasa wananchi kutowachukia na kuwaogopa kwani hivi sasa atayejaribu kurudia tabia ya ushirikina atafariki mara moja.

Hata hivyo zoezi hilo lilipata baraka kutoka kamati ya Polisi jamii na ulinzi shirikishi na kutaka wakazi hao wa Iganzo kufanya zoezi hilo kwa amani na kama kutatokea uvunjifu wa amani utatokea viongozi watawajibika.

Post a Comment

 
Top