Menu
 

Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Mtu mmoja amefariki kwa ajali mkoani Mbeya kutokana na ajali ya barabarani iliyotokea katika barabara ya Mbeya/Iringa Mei 18 mwaka huu majira ya saa 7:30 mchana.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa Advocate Nyombi amesema ajali ilitokea eneo ya Mabadaga, Wilaya ya Mbarali, ambapo dereva wa gari lenye nambari T 685 BSC aina ya Scania alifariki dunia na tingo wake kujeruhiwa, baada ya gari kugongana na gari aina ya Benz lori lenye nambari za usajili T 202 AGE  likiendeshwa na dereva Bwana God Mwakyusa (30), mkazi wa Mafinga Mkoani Iringa.

Amesema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika katika Hospitali ya Chimala Mission na pia majeruhi huyo amelazwa katika hospitali hiyo na hali yake bado ni mbaya na jina lake halijaweza kufahamika.

Kamanda Nyombi amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa gari aina ya Benz na mara baada ya kusababisha ajali hiyo dereva wa gari hiyo alikimbia kusikojulikana na uchunguzi wa ajali hiyo unaendelea.


Post a Comment

 
Top