Menu
 

Mke wa Mwenyekiti wa Kijiji wa Kijiji cha Motomoto Bi Salome Ipopo aliyeketi, ikiwa amekwepa kamera, ambaye alivuruga mkutano kwa kuporomosha matusi kwa kila mwananchi aliyekuwa akichangia hoja katika mkutano wa hadhara baada ya mumewe kutuhumiwa kuuza ardhi ya kijiji na kufuja pesa za mradi wa maji.
Wananchi wa Kijiji cha Motomoto wakielekea katika mkutano wa hadhara wa kijiji hicho.
Wananchi walioitikia wito wakiwa wameshikwa na butwaa na wakiwa hawajui kinachoendelea baada ya Mwenyekiti wa Kijiji cha Motomoto Bwana Kassim Mwagala kukana shutuma za kuuza ardhi ya kijiji.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Motomoto Bwana Mwagala, aliyevalia kofia nyeupe akikwepa kupigwa picha.
Kufuatia majibizano hayo wananchi hawakuridhishwa na majibu ya Mwenyekiti na kwamba agenda nyingine zilifichwa hali iliyosababisha wananchi kugoma kuendelea na mkutano na kiongozi huyo kuahirisha mkutano, huku wananchi wakimzomea na kumtaka yeye na serikali yake kujiuzuru mara moja, kitendo ambacho alikipinga na kudai kwamba agenda hizo ziletwe ili mkutano uitishwe siku nyingine.(Picha na Ezekiel Kamanga).

Post a Comment

 
Top