Menu
 

Baadhi ya Askari wa Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya.
*******
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Jeshi la polisi Mkoani Mbeya limelazimika kufanya kazi ya ziada kumuokoa mwanamke aliyefahamika kwa jina la Hawa Mwalongo (30), mkazi wa Mtaa wa Mwambenja, Kata ya Iganzo, Jijini Mbeya.

Tukio hilo limetokea Mei 4 mwaka huu majira ya Alfajiri mtuhumiwa akiwa na mwanae Alfonce Mwalongo (miezi mitano), alikutwa akiwa uchi huku mwanae huyo akiwa mita chache kutoka kwenye nyumba aliyopanga inayomilikiwa na Bwana Mashaka Seke.

Mmoja kati ya mashuhuda ambaye ni jirani yake amesema walisikia mtoto akilia alfajiri ndipo waliamua kutoka nje na kumkuta Bi Hawa akiwa mtupu na walipomsemesha, alisema anatoka Bunju Dar es salaam na kwamba anelekea Mbeya na alipoulizwa nguo zipo wapi hakuwa tayari kueleza na kutoelewa kinachoendelea.

Ameongeza kuwa amesafiri na lori lililokuwa na Container na kufika hapo baada ya kufukuzwa na baba yake mlezi aitwaye Esco Sikazwe, baada ya kutelekezwa na mumewe Bwana Nikas Mwalongo.

Uchunguzi umebaini kuwa mwanamke huyo alitelekezwa na mumewe kutokana na ujauzito wa mwanawe Alfonce, kisha kuhamia kwa baba yake mlezi ambaye alimfukuza kutoka Mtaa wa Mwakibete jijini hapa hali iliyomlazimu kwenda kupanga eneo la Ilemi majuma mawili yaliyopita.

Kwa upande wake Balozi Lukas Mwakalonge alitoa taarifa kituo cha polisi majira ya saa moja asubuhi, eneo la tukio na kumchukua mwanamke huyo na wanawe wawili Seif Mwalongo (2) na Alfonce na kuondoka nao na kwenda Kituo cha Polisi Kati baada ya wananchi wenye hasira kali kutawanywa na Polisi ambao walikuwa na nia ya kumpiga mwanamke huyo.


Aidha, amesema kuwa alimpokea Bi Hawa baada ya kuletwa na Peter John ambaye walikuwa wanafanyakazi pamoja katika moja ya Vyuo vikuu jijini Mbeya kama mhudumu wa mazingira katika chuo hicho.

Hata hivyo Bibi Mmoja Sandubwe Nabwike (90) ameowaonya wananchi kutojichukulia sheria mkononi kwani kufanya hivyo kutasababisha mauaji kwa wananchi wasiokuwa na hatia kwani hata yeye ameshawahi kuzushiwa kuwa ni mshirikiana na kutengwa, lakini baada ya uchunguzi akabainika kuwa si mchawi.

Hili ni tukio la tatu kwa wanawake kuhisiwa ni washirikina lakini baada ya kufikishwa hospitalini ilibainika kuwa ni wagonjwa wa akili, akiwemo Mwalimu mmoja aliyewahi kusoma Chuo Kikuu cha TEKU.


Post a Comment

 
Top