Menu
 

Chifu Kiongozi wa Kabila la Kisafwa Bwana Roketi Mwanshinga(Kulia) akiongoza jopo la Machifu kuweka tambiko la kukemea vitendo vinavyohusisha na Imani za kishirikiana katika Shule tatu za Msingi katika Kata ya Itenzi.
Chifu Kiongozi wa Kabila la Kisafwa Bwana Roketi Mwanshinga(pichani kushoto ) akiongoza jopo la Machifu kuweka tambiko la kukemea vitendo vinavyohusisha na Imani za kishirikiana katika Shule tatu za Msingi katika Kata ya Itenzi na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Tambukareli (pichani kulia) .
Machifu wakiingia katika Ofisi ya Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi ya Tambukarelikufanya tambiko la kukemea vitendo viovu vinavohusishwa na Imani za kishirikina katika Shule tatu za Msingi, zilizopo Kata ya Itenzi.
Machifu wakiingia katika madarasa na kufanya tambiko la kukemea vitendo viovu vinavohusishwa na Imani za kishirikina katika Shule tatu za Msingi, zilizopo Kata ya Itenzi.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Igombe wakiwasikiliza Machifu licha ya mvua kubwa iliyokua ikiendelea kunyesha, katika zoezi la tambiko la kukemea vitendo viovu vinavyohusishwa na Imani za kishirikina.
Wananchi waliojitokeza kutoka Kata ya Itenzi katika zoezi la Machifu waliofika katani hapo kutambika kwa lengo la kukemea vitendo viovu vinavyohusishwa na Imani za kishirikina. 
********
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Machifu wa kabila la Kisafwa Mkoani Mbeya waliamuru kusitishwa kwa masomo kwa siku moja katika Kata ya Itenzi Jijini Mbeya, kutokana na wanafunzi wa jinsia ya kike kuanguka, kupoteza fahamu na kuwanyong’oshesha nguvu.

Tukio hilo limehusisha Shule za msingi za Gombe, Tambukareli na Mwasote, zoezi lililofanya na Chifu kiongozi wa kabila hilo Roketi Mwanshinga, akisaidiana na zaidi ya mchifu 30.

Pia zoezi hilo limehudhuriwa na Diwani wa Kata ya Itenzi Mheshimiwa Frank Mayemba na Askari wa Jeshi la Polisi na Ulinzi shirikishi L.M Kiyeyeu Aprili 2 mwaka huu.

Kabla ya kuanza kazi hiyo iliyohudhuriwa na mamia ya wananchi wanaozizunguka shule hizo, Chifu Mwanshinga alishusha lawama kwa Wachungaji wa madhehebu na makanisa mbalimbali Mkoani hapa, kutokana na kupokea waumini kwa kivuli cha kuokoka bila kuwauliza machifu.

Amesema kwani wao wanafahamu hawajaacha tabia zao za awali ndio maana vitendo hivi vimekuwa vikiongezeka siku hadi siku huku makanisa hayo yakichipuka kama uyoga.

Chifu Mwanshinga ameenda mbali zaidi kwa kusema daima maisha yao ni duni, hivyo hufanya vitendo hivyo kwa nia ya kujipatia pesa wanajidanganya kwani pesa hupatikana kwa kufanya kazi kwa bidii na si vinginevyo.

Mkusanyiko huo umefanyika baada ya watoto wanaosoma katika shule hiyo hususani wasichana darasa la tano ndio wanaoathirika zaidi na ugonjwa wa kuanguka na kupoteza fahamu na kuwanyong’onyesha nguvu na hivyo kushindwa kuendelea na masomo na kuwapeleka nyumbani kwao.

Katika mkutanoi huo Machifu wameagiza yeyote anyejihusisha na masuala hayo aache mara moja na kutoa onyo yeyote atakayekaidi agizo hilo atatembea barabarani akiwa kichaa.

Aidha katika hali ya kusafisha mazingira hayo machifu wote walipita katika madarasa yote ya shule zote tatu na kwamba kuanzia sasa watapiga kambi kwa muda wa juma moja hatimaye kukomesha kabisa vitendo hivyo ambavyo huathiri huduma za maendeleo ya elimu na kiuchumi mkoani hapa.

Kutokana na kukerwa na suala hili machifu wameagiza wazazi wote wakeshe kwenye shule hizo ili kukomesha kabisa vitendo hivyo.

Kwa upande wake pia Afisa Mtendaji wa Kata hiyo Bwana Deusdedit Maseke amewashukuru wazazi kwa kuitikia wito wa kufika shuleni hapo na kuonesha jinsi walivyokerwa na jambo hilo.

Shule kadhaa mkoani Mbeya zimekubwa na janga la ushirikina na kupelekea kufungwa kutokana na vitendo vya kishirikina ikiwemo Shule ya Juhudi iliyopo kata ya Iganzo ambapo Ofisi ya Mwalimu Mkuu alisilibwa kinyesi pamoja na ofisi nyingine ya walimu mbali ya kusilibwa kinyesi vyombo vya chakula vilitapakaa kinyesi.

Post a Comment

 
Top