Menu
 


 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda akiongea na wananchi pamoja na wafanyakazi wa Kiwanda cha Marumaru, Jijini Mbeya jana wakati wa ziara yake ya siku tatu.
*******
 Habari na Mwandishi wetu.
Waziri Mkuu, Mizengo Peter Pinda amewasili mkoani Mbeya kwa ziara ya siku tatu ambapo baada ya kupokea taarifa ya mkoa alisema kuwa suala la uuzaji wa kahawa mbichi liachwe mikononi kwa wakulima wenyewe kutokana na kwamba hasara na faida ya zao hilo ipo juu yao.

Aidha Pinda amesema kuwa suala la ujenzi wa miundombinu kwa mkoa wa Mbeya linaangaliwa kwa umakini zaidi ambapo ujenzi wa uwanja wa ndege unatarajia kukamilika hivi pundu kutokana na serikali kuwa na imani kuwa kukamilika kwake kutauwezesha mkoa kupiga hatua katika nyanja mbalimbali ikiwemo kilimo.

Akiwa katika kiwanda cha nyama cha Tanganyika Pekers kilichopo katika kata ya utengule Usonge wilaya Mbeya vijijini waziri mkuu Pinda amesema kukamilika kwa kiwanda hicho kutawezesha ajira kwa zaidi ya vijana 2000 na kuongeza kuwa kukosekana kwa mwekezaji wa kiwanda hicho kumechangia kuchelewa kwa utendaji kazi wa kiwanda hicho.

Wakati huohuo wamewataka wamiliki wa vindanda vya kusindika nyama na mazao mbalimbali kuwatumia wakulima na wafugaji wadogo ili waweze kunufaika kupitia shughuli zao.

Post a Comment

 
Top