Menu
 

Habari na Angelica Sullusi, Mbeya.
Jiji la Mbeya na vitongoji vyake limekumbwa na uhaba mkubwa wa mafuta ya taa, hali ambayo imesababisha kero kubwa kwa wananchi wanaotegemea nishati hiyo kwa matumizi mbalimbali.

Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wetu, ulibaini kuwa vituo karibu vyote vya mafuta Jijini hapa vilikuwa vikiuza mafuta aina ya petroli na diseli pekee, huku mafuta ya taa yakiwa hayapatikani.

Baada ya kutembelea vituo vingi vya kuuza mafuta ilibainika kuwa kituo kimoja tu kilichopo eneo la Mbalizi nje kidogo ya Jiji ndicho ambacho kilikuwa kinauza mafuta ya taa, huku kikionyesha kuelemewa na wingi wa watu wanaotafuta mafuta hayo.

Baadhi ya watu waliozungumzia kadhia hiyo wamesema kuwa mafuta ya taa yameadimika Jijini hapa kwa muda wa wiki mbili sasa na kadri siku zinavyozidi kwenda ndivyo hali ya upatikanaji wa mafuta hayo inazidi kuwa mbaya.

Mzee Gidion Mwalusaka amesema kuwa analazimika kutoka Inyara umbali wa kilometa 25 kutoka katikati ya Jiji la Mbeya kuja mjini kutafuta mafuta ya taa na hata alipofika mjini imemchukua muda mrefu kupita kwenye vituo mbalimbali vya mafuta kuyatafuta.

Post a Comment

 
Top