Menu
 

Habari na Pulkeria Kisoka, Mbozi.
Mwanafunzi wa Kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari ya Kutwa Mlowo, Wilaya ya Mbozi, Mkoani Mbeya Tabu Mfyeti, amefukuzwa shule baada ya kukutwa akinywa pombe darasani na wengine 9 wakiwa kwenye uchunguzi na maamuzi ya bodi.

Akiongea na mwandishi wetu Mkuu wa shule hiyo Mwalimu Sufyan Msarilwa, amesema mwanafunzi huyo ni wa kike na alikutwa akinywa pombe na amekuwa akifanya hivyo mara kwa mara wakati wa masomo pamoja na wenzake hao 9 ambao wanaendelea kuchunguzwa.

Kwa upande wake mwanafunzi huyo Tabu amekiri kutenda kosa hilo na kwamba amekuwa akinywa pombe kwa madai ya kuwa hawezi kusoma bila kufanya hivyo.

Hata hivyo jitihada za wazazi wa mwanafunzi huyo kuuomba uongozi wa shule hiyo kumsamehe mtoto wao zimegonga mwamba kutokana na kile kilichotamkwa na uongozi huo kuwa wamechoshwa na tabia chafu za mwanafunzi huyo.

Post a Comment

duduu said... 19 May 2012 at 02:58

Kwa maoni yangu kama Mwalimu kumfukuza Mtoto skuli kwa kufanya kosa kubwa kama hili ambalo upo uwezekano wa kumsahihisha na Mwanafunzi kurudi katika hali ya kawaida ni Upumbavu wa Wizara yetu ya Elimu na Mafunzo, na huyo Mwalimu itakuwa ame...kosa hekima ya uwajibikaji wa kufunza tabia na kuelimisha , kumfukuza kijana skuli bila kumrekebisha ni kwenda kumpeleka mitaani kuzurura , kukosa ajira na hapa unaliingizia Taifa mzigo wa ukosefu wa ajira, unazidisha ajira za vibaka na wizi na ujambazi,unalizidishia Taifa idadi ya watu wasiojua kusoma na kuandika, ELIMU NI UFUNGUO WA MAISHA, TAIFA LINAJENGWA NA VIJANA, KUMBOMOLEA KIJANA MSINGI WAKE WA MAISHA NI KULIBOMOA TAIFA. ZINDUKENISee More

Chimbuko Letu said... 19 May 2012 at 03:34

Shukradi sana@Duduu ama hakika huu ujumbe utamfikia mhusika na bila shaka na ungana na wewe ili kuhakikisha mtoto huyu anapata haki yake ya msingi na ya umuhimu ambayo ni Elimu, Mwalimu kwa kufanya hivi au jambo ulilolitumia ni nzito sana kwa sababu umempotezea mwanafunzi wako future. Shukrani tunaamini maombi yetu yatapewa kipaumbele

 
Top