Menu
 

HASSA ft ASLAY - VOCHA  
DOGO GULLAMUH - NG'OMBE
  
Ngoma hii yaitwa Ng'ombe yake Dogo Gullamuh,ambaye ni bwana mdogo mwenye umri wa miaka 14 toka Mbeya Tanzania, ambapo yafanana na ile ngoma iitwayo Vocha yake Hassan akishirikiana na Dogo Aslay na imezua utata na kuwepo kwa maswali mengi toka kwa wadau/wasikilizaji.

Swali lililopo:- Kama tunauchungu wa kufika soko la kimataifa kwa staili hii muziki wa Bongo Fleva utakuwa au tutazidi udidimiza? na ni yupi mmiliki halali na nani kamcopy mwenzie? Ngoma hii Idea ni ile ile na style ya uimbaji ni ile ile, Kilichobadilika ni neno VOCHA na NG'OMBE lakn mashairi ni yale yale!!

Ngoma hii aliletewa kwa mwanangu ambaye tunafanya naye Show ya Kali za Bomba hapa Bomba FM Radio 104.0Mhz Mbeta kwa Shebby Laizer na kunikabidhi niweze sikiliza, ndipo tuliposhitukia kuwa inautata.

Lakini kwa mujibu wa Producer wa ngoma hii Zest Mkali toka Mojamoja Records iliyopo Jijini Mbeya, adai kuwa yeye haifahamu ngoma ya Vocha yake Hassan. 


Artist:- Dogo Gullamuh
Song:- Ng'ombe
Studio:- Mojamoja Rec
Producer:- Zest Mkali.

From:- Greyson Salufu Chatanda a.k.a Chris Bee
          Bomba FM Radio 104.0Mhz.
Mbeya Tanzania.
Kali za Bomba & Bomba Special Show.
+255655117664.

Post a Comment

 
Top