Menu
 

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mheshimiwa Abbas Kandoro katika picha ya pamoja na Waandishi wa habari mkoani Mbeya, nje ya Ukumbi wa Itemba Village mara baada ya kumalizika kwa Kongamano la Uhuru wa Vyombo vya habari.
******
Habari na Angelica Sullusi, Mbeya.
Waandishi wa habari Mkoani Mbeya wametakiwa kuandika habari zilizofanyiwa uchunguzi wa kina na zenye manufaa kwa wananchi na kuachana na habari kutoka chanzo kimoja.

Hayo yameelezwa na Mwandishi wa habari Mkongwe nchini Phill Karashani - katika semina iliyoandaliwa na Shirikisho la klabu za waandishi wa habari Tanzania(UTPC) kwa waandishi wa Mkoani mbeya juu ya habari za uchunguzi.

Akitoa mada kwa wanahabari juu ya uandishi wa habari za uchunguzi Karashani amesema kuwa wakati umefika kwa wanahabari kutumia taaluma zao vyema kwa kujikita katika kuandika habari za uchokonozi zilizojificha ambazo si rahisi mtu kuzitambua.

Jumla ya waandishi wa habari 20 kutoka vyombo mbalimbali vya habari Mkoani hapa wanahudhuria mafunzo hayo ya siku sita ambapo Katibu Tawala wa Mkoa huu Mariam Mtunguja aliyafungua mafunzo hayo juzi, Mei 14 mwaka huu.

Post a Comment

 
Top