Menu
 


Habari na Mwandishi wetu.
Wafanyakazi wa mamlaka ya maji jiji la Mbeya wameiomba Serikali kupunguza asilimia ya kodi inayokatwa kwenye mishahara yao ili fedha wanayoipata iwawezesha kujikimu kimaisha.

Ombi hilo limetolewa na mkurugenzi wa mamlaka hiyo Injiani Saimon Shauri wakati wa mahojiano na Bomba Fm kuhusu namna walivyojipanga kuadhimisha siku hiyo ya wafanyakazi.

Amesema kutokana na kukatwa asilimia kubwa ya mshahara kwa ajili ya kodi maisha ya wafanyakazi yameendelea kuwa ya kubahatisha kutokana na kipato wanachokipata kutowatosheleza katika maisha yao.

Aidha ametoa wito kwa wafanyakazi wa idara hiyo kufanya kazi wa kujituma licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali za kimaslahi kutokana na kukatwa asilimia kubwa ya kodi katika mishahara yao.

Post a Comment

 
Top