Menu
 

 Tamasha la Burudani kwa washindi wa Tuzo za Kili Music Award 2012 limemalizika kwa msanii Roma Mkatoliki kufunga pazia hilo kwa mkoa wa Mtwara. Katika Tamasha hili la jana Roma Mkatoliki amejihidhirishia dhahiri kuwa muziki wake wa Hip Hop unapendwa na kukubalika vilivyo kwa mashairi yake pale maelfu ya wakazi wa mji wa Mtwara walivyokuwa wakimshangilia na kuikubali show yake kiasi cha kutaka aendelee licha ya muda kumalizika uwanjani hapo kwa wasanii hao kutoa burudani.
 Roma akiwa jukwaani akipagawisha vilivyo...
 DJ Choka akiimba viitikio vya nyimbo za Roma jukwaani
 DJ Choka akiscrach na kuimba huku DJ Makey wa EATV na EAR akiwa kando yake.
 Roma aliamua kugawa CD za Nyimbo zake ili mziki huo wa Hip Hop ukasikilizwe kila kona.
Kidole cha Mwisho juuuuuu!!! Ndivyo mashabiki walivyokuwa wakimwitikia Roma Mkatoliki wakati akitumbuiza jukwaani na kufunika mbaya show ya Mtwara kwani hata baada ya kushuka lakini bado walimhitaji kuendelea.
Ali Kiba akimsindikiza Ommy Dimpoz katika wimbo aliomsaidia wa Nai Nai na hatimaye kumpa tuzo mbili.
Mzee wa Pozz kwa Pozz Ommy Dimpoz akilishambulia jukwaa na nyimbo zake za Nai Nai na Baadae
Mwimbaji wa Nyimbo za Bongo Fleva Ali Kiba akishambulia jukwaa na vijana wake.
Queen Darling akiwajibika jukwaani ndani ya uwanja wa Umoja mjini Mtwara jana usiku.
Mkali wa masauti Barnaba akifanya vitu vyake jukwaani.
Mkali wa miondoko ya kipwani kutoka Zanzibar AT akifanya vitu vyake sambamba na wanenguaji wake wakati wa tamasha la Washindi wa Tuzo za Kilimanjaro “Kili Music Award Winners Tour” inayofanyika katika uwanja wa Umoja mjini Mtwara. Wasanii kadhaa walipanda jukwaani.
Mkongwe wa Taarab, Bi Hadija Kopa akitumbuiza jukwaani na kukonga nyoyo za wakazi wa Mwambao wa Pwani ya Bahari ya Hindi Mkoani Mtwara kwa vibao vyake kadhaa ambavyo vimempa tuzo ya Kili Music  Award 2012
Show ya wakali wa Kili Music Award 2012 ndani ya Uwanja wa Umoja mjini Mtwara ndio imeanza sasa. Pichani ni Mshindi kutoka Mtwara ambaye ataenda kurecord jijini Dar es Salaam Nicolazo akitumbuiza na kuwashinda wenzake wawili.
 Chipukizi wa 3 wa Mtwara waliokuwa wakichuana kutafuta mmoja atakaeenda Kurecord jijini Dar es Salaam kwa udhamini wa Kilimanjaro Lager
 Mashabiki wakifuatilia show hiyo ya kutafuta vipaji.

Shangwe za kumshangilia Chipukizi ambaye ni kipaji kipya cha Kili Music Award kutoka Mtwara. Kwa hisani ya FATHER KIDEVU

Post a Comment

 
Top