Menu
 

Warembo watakaoshiriki shindano la Miss Redd's Mbeya 2012, siku ya Ijumaa June 1, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Mkapa kwa kiingilio cha shilingi 10,000 kwa viti maalum na shilingi 5,000 kwa viti vya kawaida.
Shindano hili limedhaminiwa na TBL kupitia kinywaji chake cha Redds, SBC Tanzania LTD kupitia kinywaji cha Mountain Dew, Masasi Fashion, Access Computer LTD, Beaco Resort, Grace College, Shaba Pub na Mfikemo Hotel na litasindikizwa na burudani toka kundi la Coast Modern Taarab a.k.a Watafiti wa mipasho.
 Warembo wanaoshiriki Miss Redds Mkoani Mbeya wakiwa wanapita mbele ya waandishi wa Habari mapema jana.
 Mratibu wa Mashindano ya Miss Redds Mbeya Amani Mbilo akiongea na waandishi wa Habari kuhusiana na Malengo ya kumpata Miss Redds atakae shindania Miss kanda za Juu kusini na Hatimaye kumpata miss Redds Tanzania
 Mhariri wa Bomba FM ndugu Gabriel Mbwilo ambao ni waandaaji wa Miss Redds Mbeya akiwatambulisha ma miss hao ambao waku jumla ya 12 kutoka wilaya za jiji warembo 5, Mbeya vijijini warembo 3 , Mbalali 1, Chunya 1 na Mbozi mshiriki 1.
 MMoja wa wadhamini wa Miss Redds Mbeya Ndugu Samwel Mtela Mkurugenzi wa Access Computers akiwaeleza waandishi kwamba atatoa Laptop ya kisasa yenye Thamani ya Shiringi laki saba za kitanzania kwa mshindi wa kwanza.
Waandishi Mbali mbali walikuwepo katika eneo hilo jana (Picha na Joseph Mwaisango).

Post a Comment

 
Top