Menu
 

Jay-Z na Will Smith wameunga mkono mawazo ya Barack Obama kuhusu kusupport ndoa za jinsia moja nchini Marekani.

Will alisifia tamko la Obama kuwa ni la kijasiri katika mwaka wa uchaguzi nchini Marekani.

"Kama mtu yoyote akipata mtu wa kuwapenda na kuwasaidia katika kitu hiki kigumu kiitwacho maisha, ntamuunga mkono kwa namna yoyote"alisema Will alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mjini Berlin.Kwa upande wake Jay-Z anaamini kuwa wapenzi wa jinsia moja wanapaswa kuwa na haki ya kuoana.

"Nadhani ni jambo la haki kufanya.... hata kama itamnyima kura ama la. Nimekuwa nikifiria hiki ni kitu kilichokuwa bado kinairudisha nyuma nchini" alisema Jigga.
"Kile watu hufanya majumbani mwao ni suala lao wenyewe na unaweza kuchagua kumpenda yoyote unayempanda" Haina tofauti na ubaguzi wa watu weusi. Ni ubaguzi wa wazi".
Tamko hilo la Barack Obama limepokelewa kwa hisia tofauti Marekani na kwingineko duniani huku wengine wakimpinga vikali.

Post a Comment

 
Top