Menu
 

Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Wimbi la mauaji ya watu kufariki katika mazingira ya kutatanisha limezidi kushika kasi Mkoani Mbeya.

Mnamo Mei 3 mwaka huu majira ya saa tatu asubuhi uliokotwa mwili wa mtu mmoja jinsi ya kiume anayekadiriwa kuwa na umri wa kuanzia miaka 25 hadi 30, ukiwa na majeraha mbalimbali sehemu za mwili wake.

Aidha, marehemu anasadikika kupingwa na vitu butu hali iliyompelekea kuvuja damu nyingi mwilini mwake.

kwa upande wake Kaimu Kamanda wa Polisi wa mkoa Barakiel Masaki, amesema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa iliyopo jijini Mbeya na upelelezi wa tukio hili unaendelea na hakuna mtu yeyote aliyekamatwa kuhusika na tukio hili.

Hata hivyo kuuawa mtu huyo ni mfululizo wa matukio mengi yaliyotokea hivi karibuni mkoani hapa, licha ya Jeshi la Polisi  kuimarisha ulinzi kwa kutumia dhana ya polisi jamii na ulinzi shirikishi.

Kutokana na adha ya mauaji, upigwaji nondo kwa baadhi ya mitaa na kata mkoani hapa kumeanzishwa ulinzi wa sungusungu ili kupunguza vitendo vya mauaji, ambapo baadhi ya hivyo vinahusishwa na imani za kishirikina.

Post a Comment

 
Top