Menu
 

Habari na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
Mkulima na mkazi wa Kijiji cha Iziwa Wilaya ya Mbeya Vijijini Bi.Eva Tume(38),amefariki dunia baada ya kukusanya nguo zote na vyombo vyote ndani ya nyumba kisha kufunga mlango na kujichoma moto na kuteketea mwili wote.

Tukio hilo limetrokea Juni 26 mwaka huu,majira ya saa 12 jioni mara baada ya mumewe aitwaye Tume Mwalingo,ambaye ni mlinzi kuondoka nyumbani hapo na kuelekea kazini.

Aidha Mwenyekiti wa Kitongoji cha Iwambala Bwana Asikile Mtafya,amesema siku hiyo majira ya mchana marehemu alionekana maeneo kadhaa akiwa mwenye hasira.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya Diwani Athuman,amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba marehemu alikuwa akisumbuliwa pia na ugonjwa wa akili ambapo alikuwa akihudhuria kliniki katika Hospitali ya Rufaa kwa jalada namba 30/33/26.

Ametoa wito kwa wananchi walio na wagonjwa wenye matatizo ya akili kuwa nao karibu zaidi na uangalizi mzuri ili kuokoa maisha yao badala ya kuwaacha wao wenyewe.

Hata hivyo,Kamanda Diwani amesema uchunguzi umefanikiwa na mwili wa marehemu ulikabidhiwa kwa nfugu wa marehemu kwa ajili ya mazishi yaliyofanyika Juni 17 mwaka huu..

Post a Comment

 
Top