Menu
 

Habari na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
Mkazi wa Mtaa wa Isangu,Wilaya ya Mbozi,Mkoani Mbeya Bwana Joseph Kalinga(28),amehukumiwa kwenda jela miezi 10 au kulipa faini ya shilingi 300,000 baada ya kupatikana na halia ya kumlisha kinyesi cha binadamu Bwana Musa Kilalawima.

Kesi hiyo iliyoanza kusikiliza tangu Machi 26 mwaka huu,katika mahakama ya wilaya hiyo chini ya Mwendesha mashtaka Lugano Alfred ambapo imedaiwa Machi 10 mwaka huu,majira ya saa 8 mchana mtaani hapomtuhumiwa akiwa na mwenzake walimlisha kinyesi hicho mlalamikaji.

Aidha mwenzake hajakamatwa na kosa hilo ambalo ni kinyume cha sheria kifungu cha 241 sura ya 16.

Akisoma mashtaka Hakimu wa wilaya hiyo Bi. Martha Malimi alimtaka mtuhumiwa kulipa shilingi 100,000 kwa serikali na shilingi 200,000 kama faini ya mlalamikaji.

Hata hivyo kabla ya hukumu mwendesha mashtaka alitaka itolewe adhabu kali kwa mtuhumiwa kutokana na kitendo hicho.

Kwa upande wake mlalamikaji akiwa nje ya mahakama alieleza kutoridhika na hukumu hiyo na kwamba atakata rufaa kupinga hukumu hiyo ili iende ngazi ya juu ya kimahakama.

Post a Comment

 
Top