Menu
 

Habari na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
Mkazi mmoja wa Kitongoji cha Ihenga,Kata ya Isuto,Wilaya ya Mbeya Vijijini Bwana Hoswe Hansuli(70),amejikuta akiishi kwa wasiwasi kufuatia mawe ya ajabu kumpiga akiwa chumbani kwake.

Tukio hilo la ajabu limemkubwa kwa takribani juma moja sasa hali iliyomfanya mkewe kuondoka nyumbani na kwenda Songwe,kukimbia adha hiyo ya aina yake.

Mbali na ya kikongwe huyo kupingwa mawe na matofali ya ajabu,pia vyombo vyake vingine kama redio navyo vimekuwa vikibondwa.

Katika sakata hilo wachungaji wawili ambao majina yao hawakuwa tayari kuyataja walifika hapo kwa nia ya kufanya maombi ili kumwondolea bughudha mzee huyo,juhusi ambazo ziligonga ukuta ambapo nao walitimua mbio kukwepa mawe hayo ya ajabu.

Uongozi wa Kijiji cha Isuto ulimwita Mzee Hoswe kutaka kujua kulikoni,ambapo naye alijibu haelewi chochote.Ingawa sakata hilo linahusishwa na imani za kishirikina japo Mzee huyo kakanusha kujihusisha na vitendo hivyo na kuwaomba wananchi kuwa endapo kafanya kosa lolote anaomba asamehewe kwani adhabu anayopata ni kubwa kwake na kumnyima kabisa usingizi.

Post a Comment

 
Top