Menu
 

 
  Basi aina ya Coaster lililokuwa linatokea Jijini Mbeya kuelekea Wilaya ya Kyela Muda mfupi baada ya Ajali kutokea.
 Gari la Mizigo ambalo limehusika na ajali hiyo likiwa pembeni muda mchache baada ya ajali hiyo kutokea.
 Baadhi ya waandishi wa Habari wakiwa Hospitali ya Rufaa Jijini Mbeya muda mchache uliopita.
 Mmoja wa majeruhi ambae ameshapata matibabu.
 Mmoja ya binti ambae ameumia Vibaya akipata matibabu  katika hospitali ya Rufaa muda mchache uliopita.
 Baadhi ya Ndugu jamaa na marafiki waliofika eneo nyumba ya Kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Rufaa kuwatambua ndugu zao muda mchache uliopita
Polisi wa usalama wa Barabarani wakiwa katika hospitali ya Rufaa Mbeya(Picha na Joseph Mwaisango wa Mbeya Yetu). 
*******
Abiria 10 kati ya 30 waliokuwemo katika Coaster iliyokuwa ikitokea Uyole jijini Mbeya, kuelekea Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya wanadhaniwa kufariki na wengine 19 wamejeruhiwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Rufaa iliyopo jijini hapa baada ya  kugongana uso kwa uso na gari la mizigo aina Lori.

Tukio hilo limetokea eneo la kona huko Igawilo ambalo, jiji hapa ambapo abiria 8 na dereva wa Coaster wamefariki wakati katika gari ya mzigo mtu mmoja naye amefariki...... 

*****Kwa habari zaidi endelea kufuatilia mtandao huu******.

Post a Comment

 
Top