Menu
 

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),alipokuwa ametembelea Chuo Kikuu Cha Teofilo Kisanji(TEKU).
*******
 Habari na Angelica Sullusi,Mbeya.
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema bado kinaendelea na mchakato wa kuwaondoa madarakani wanachama wake wenye tuhuma za ufisadi na wale wasiokuwa na maadili mazuri kwa jamii, maarufu kwa jina la kuvua gamba.

Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nauye Jijini Mbeya alipozungumza na waandishi wa habari Jijini hapa.

Nape amesema kuwa dhana ya kujivua gamba ilipangwa kuwa na awamu tatu, ambapo awamu ya kwanza ya kuwataka wahusika wawajibike wenyewe na imepita ingawa ilikuwa na mwitikio mdogo.

Kwa mujibu wa Nape awamu ya pili ya kujivua gamba ilipangwa kufanyika kupitia uchaguzi wa ndani ya chama hicho, na kuwa awamu hiyo ndio sasa inaendelea.

Amesema awamu ya tatu ni ya kuwawajibisha wahusika kupitia vikao vya chama, ambapo mpaka sasa tayari vikao vya kuwajadili viongozi wa juu wa chama hicho wenye tuhuma za ufisadi vimeanza na vitakapokamilika umma utashuhudia mageuzi makubwa ya uongozi wa chama hicho kikongwe nchini.

Aidha, Nape amesema katika awamu ya pili ya kujivua gamba ambayo inahusisha wanachama wote kutoa maamuzi kupitia uchaguzi, mchujo mkali utapitishwa kwa watakaoomba kugomea nafasi mbalimbali za uongozi, ambapo wale wenye tuhuma majina yao hayatarudi.

Post a Comment

 
Top