Menu
 


Eden Hazard
Hazzard ajiunga na Chelsea kutoka Lille
Klabu ya soka ya England ya Chelsea imetangaza katika tovuti yake kwamba hatimaye imekubaliana na klabu ya Lille ya Ufaransa kwamba mchezaji wa kimataifa ya Ubelgiji, Eden Hazard, atajiunga na klabu hiyo ya Stamford Bridge msimu ujao. Mchezaji huyo, mwenye umri wa miaka 21, tayari afya yake imekaguliwa na klabu ya Chelsea, na imeonekana hana tatizo lolote.

Walipochukua ubingwa wa ligi ya klabu bingwa, nilijiuliza, "Kwa nini sio Chelsea?", alisema Hazard.
"Kulikuwa na mvutano kati ya Chelsea na Manchester united, lakini binafsi naona Chelsea ndio mradi bora zaidi. Ni klabu cha ajabu."

Inaarifiwa kwamba Chelsea wameamua kutoa pauni milioni 32 kumpata kijana huyo, na ambaye akizungumza na kituo cha redio cha nchini Ufaransa, RMC, aliongezea: "Chelsea ni timu changa, na nitakuwa na nafasi bora zaidi ya kucheza."

"Ikiwa nitajitahidi kucheza vyema nikiwa Chelsea, huenda nikapata nafasi katika timu."

Hazard alikuwepo katika kikosi kilichoshinda ligi wakati Lille ilipopata ubingwa mwaka 2010-11 na katika msimu wake wa mwisho, alifanikiwa kufunga magoli 21 katika mechi 48.

Katika mechi yake ya mwisho dhidi ya Nancy mwezi uliopita, alifanikiwa kupata hat-trick (magoli matatu) wakati timu yake ilipocheza dhidi ya Nancy. Lakini alishindwa kuvuma wakati Ubelgiji iliposhindwa na England katika mechi ya kirafiki Jumamosi iliyopita.

Hiyo ilikuwa ni mara yake ya 28 kuichezea timu yake ya taifa ya Ubelgiji. Hazard sasa ni mchezaji wa pili kusajiliwa Chelsea tangu dirisha la usajili la mwezi Januari, wa kwanza akiwa ni mchezaji wa kimataifa wa Ujerumani, Marko Marinas.

BBC

Post a Comment

 
Top