Menu
 

Habari na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU),kimepata uongozi mpya kupitia uchaguzi mkuu uliofanyika chuoni hapo mapema mwezi huu,baada ya viongozi wa awali kumaliza muda wake,kwa mujibu wa katiba ya chuo hicho.

Rais Mstaafu Ambukeghe Imani amemaliza kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wa chuo hicho akishirikiana na Baraza lake la mawaziri.

Aidha,Tume ya uchaguzi iliteuliwa kusimamia uchaguzi huo ikiongozwa na Mwenyekiti wake Bwana Emmanuel Mkavenga,ambapo mchakato wa uchaguzi ulitangazwa mapema mwezi uliopita na watu kadhaa walijitokeza kugombea nafasi mbalimbali ikiwemo ya Urais,makamu urais na wabunge.

Awali uchaguzi ulifanyika Mei 29 na matokeo kutangazwa Mei 30 mwaka huu,ambapo Bwana Godbless George alitangazwa kuwa mshindi wa ngazi ya Urais.

Kufuatia ushindi huo Tume ilipokea rufaa kutoka kwa baadhi ya wagombea Rais pamoja na makamu wake wana itikadi ya vyama hali iliyopelekea tume kutengua matokeo hayo na kuitisha uchaguzi upya  baada ya kupata maoni kutoka kwa Uongozi wa Chuo.

Bwana Steven Lespidius alichaguliwa baada ya kupata kura 454 na kuwashinda Myombo Mawazo na Swebya Hongera ambao wote walipata kura 193 wakati kura 109 ziliharibika na jumla zilipingwa kura 949.

Kiti cha Makamu Rais alichanguliwa Deus Petro na wote kuapishwa Juni 14 mwaka huu katika Ukumbi mpya wa TEKU na mwanasheria wa Wilaya ya Mbeya Prosper Msivala ambapo aliwataka viongozi hao kuongoza wenzao kwa mujibu wa katiba ya chuo hicho.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo Profesa Tuli Kasimoto,kufanya kile kilichowaleta chuoni hapo,badala ya kujihusisha na masuala ya siasa na kuvionya baadhi ya vyama vya siasa kutoingilia katika chuo hicho kupenyeza siasa kwani kwa kufanya hivyo ni kuwatenganisha wanachuo na kwamba wao wapo kama familia moja.

Hata hivyo amemalizia kwa kusema utawala utatoa ushirikiano ili kudumisha mshikamano chuoni hapo.

Post a Comment

 
Top