Menu
 

Na. Shomi Mtaki, Tunduma
Tabia ya viongozi wa Chadema kuchanganya masualaya yaushabiki wa kisiasa na kufitinisha wananchi na viongozi wa Chama  Cha Mapinduzi (CCM) katika mikutano yake vya hadhara pamoja na vikao vya baraza la halmashauri ya mji wa Tunduma wlayani Momba, nusura kiongozi mmoja wa chama apate kipigo.

Kiongozi huyoi Frank Mwakajoka ambaye ni diwani wa kata ya Tunduma (Chadema), alinusulika kipigo hichojana  kutoka kwa wajumbe wa Baraza la Halmashauri ya Mji huo baada ya kuwatukana wajumbe katika kikao hicho kilichafanyikia ndani ya ukumbi wa hoteli ya Flamingo mjini hapa.

Tukio hilo lilitokea katika kikao hicho kufuatia hoja ya mwenyekiti wa mtaa wa Tukuyu Kenneth Mwankuga, kutaka ufafanuzi wa kauli za viongozi wa Chadema, kudai katika mkutano wa hadhara uliofanyika hivikaribuni katika mtaa wake kuwazushia uongo viongozi wa  CCM kuwa wameuza soko la Majengo.

 Mwankugha alisema viongozi hao akiwemo diwani huyo walifanya mkutano wa hadhara, katika eneo hilo na kuenezauzushi huo na kudai kuwa uongozi wa Chadema umepinga hatua hiyo jambo ambalo halikuwa sahihi.

Hivyo kupitia Baraza hili naomba nipate ufafanuzi ili zaidi ili niwapelekee wananchi majibu sahihi maana viongozi hao tunao katika kikao hiki,” alisema Mwankuga.

Hoa hiyo iliungwa mkono na wajumbe wengine wanaotokana na   CCM na kumtaja diwani huyo kuwa ndiye aliyetamka maneno hayo na kuwa amekuwa na tabia ya kutengeneza uchochezi kila mara   anapofanya mikutano ya hadhara mjni hapa.
 
Wajumbe hao walisema diwani huyo akishirikiana na viongozi wa chama chake, amekuwa mstari wa mbele kusababisha kutoweka kwa amani na kuzusha vurugu zisizo za msingi zinazojitokeza mara kwa mara katika mji huo

Hata hivyo maneno hayo yalimfanya diwani huyo asimame na kuanza kukanusha taarifa hiyo kwa madai kuwa yeye ndiye aliyekuwa akitetea kufuatia kuwepo kwa taarifa hizo.

Hata hivyuo diweani huyo alianza kutoa lugha chafu dhidi ya wajumbe wa mkutano huo akisema,“acheni ujinga wenu,hakuna mnachosali mtaendelea kubaki hivyo hivyo na tena nawaambieni kesho (leo) nitaitisha mkutano mwingine niwaambie wananchi ujinga wenu” alisema.

Wakati diwani huyo akiendelea kuongea, kelele za wajumbe hao na baadhi ya wa Chadema walianza mzozo huku wajumbe wengine wakiwa wamemzonga diwani huyo kwa lengo la kumpa kipigo kufuatia kauli zake hizo,ambazo hazikuwaridhisha baadhi ya  wajumbe wa baraza hilo.

Mzozo huo uliochukua takribani dakika 20, ulifanya hali ya kikao kutoeleweka ambapo baadhi ya wajumbe walitaharuki na kuwaondolea utulivu kufuatia kuendelea kulizungumzia jambo hilo badala ya kujadili agenda zilizo mbele yao.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya mji wa Tunduma Aidan Mwanshiga alikanusha kuwapo kwa jambo hilo na kuwataka wajumbe wasiingize mambo ya mtaani kwenye vikao badala yake wawe makini kujadili mambo ya msingi.
 
Akizungumzia suala hilo Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),ta ya Tunduma Hemed Steven aliwataka wajumbe hao kuacha kuingiza Siasa kwenye vikao vya maendeleo badala yake wafanye majukumu waliyotumwa na wananchi.

“Tujue siasa inatumika wapi na wapi ni masuala ya maendeleo haya yaliyotokea mimi nasema wajumbe watambue majukumu waliyotumwa na wananchi huo ndiyo ujumbe wangu sina zaidi I have no comment ”alisema Steven.

Naye Mwenyekiti wa Jimbo la Magharibi Chama cha Demokrasia na Maendeleo Joseph Mwachembe alipoulizwa kuhusu suala hilo alisema CCM watambue kuwa chadema hakiwezi kuwasifia bali kitaendelea kuwafitinisha na wananchi.

Post a Comment

 
Top