Menu
 

Kambi ya mwanamuziki kijana na mtanashati,mwenye uwezo wa kurap na kuimba kutoka familia ya YMCMB si mwingine namzungumzia DRAKE imekanusha vikali kwa msanii wao kuhusika katika timbwili lilitokea jana usiku kwenye ukumbi mmoja wa disco huko unyamwezini,huku kasheshe hilo likimtaja msanii mwingine kijana na maarufu pia CHRISS BROWN.

Picha zilisambaa mitandaoni leo zinazoonyesha kutolewa "ngeu"  kwa mwimbaji huyo wa miondoko ya r&b ambaye aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanadada RIHANNA ambaye pia ni dDIVA katika ulimwengu wa muziki na burudani kwa ujumla,huku DRAKE akihusishwa kusababisha madhara hayo kwa kumrushia chupa na chanzo kikielezwa ni kumgombania mwanadada RIHANNA ambaye inaonekana kuteka mioyo ya  vijana wawili hawa kimapenzi
.

Drake alikubali kuwepo ndani ya club ya W.I.P ya New York usiku wa kuamkia leo ila alikanusha kuhusika kwa namna yeyote katika sakata hilo,huku akidai wakati mtanange huo ukianza ye alishajikata zake maskani.


Inasemekana Drake alikuwa na mshikaji wake ambae ni mwanamuziki pia Meek Mill katika ukumbi huo,huku CHRISS BROWN nae alikuwepo ndani ya clu hiyo ya W.i.P ya  New York akila BATA zake!wote hawa walikua sehemu maalum (VIP) kwa ajili ya watu wazito ma maarufu kwenye ukumbi huo.


Ikumbukwe kuwa siku za karibuni kulizuka kupigana vijembe kwa watatu hao kwa kutumia mtandao wa jamii wa Twitter,huku ikisemekana wote watatu (Chriss,Meek na Drake) kwa nyakati tofauti walishawahi kumega RIHANA ,ilhali uhusiano wa Chriss Brown na mlimbwende huyo kuvuma zaidi na mpaka kupelekea wawili hao kufikishana kwenye ymbo vya dola baada ya kuhitilafiana,huku Chriss Brown akikutwa na hatia ya kumpiga mpenzi wake huyo wa zamani!


Shuhuda wa sakata hilo ndani ya ukumbi wa W.i.P, ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema "Meek alianza kumrushia maneno makali Chriss Brown na kusababisha zogo hilo na shika nikushike ambayo ilisababisha mwimbaji huyo wa r&b kutolewa ngeu kidevuni na kitu kinachosadikiwa kuwa ni chupa!

 Chriss Brown akionyesha jeraha alilopata jana usiku baada ya kasheshe hilo,hii picha aliituma kwenye ukurasa wake wa twitter!

Pia inasemekana
Polisi bado wanafanya uchunguzi zaidi wa swala hilo!kwani walilazimika kuitwa baada ya walinzi wa ukumbi huo kushindwa kudhibiti fujo hizo ambapo ziliwajumuisha pia wapambe wa karibu wa masuper star hao.

Chupa zilirushwa,viti vilivunjwa,vioo hali kadhalika kiasi cha kuifanya sehemu ya VIP ya ukumbi huo kuwa kama dampo la vingunguti hivyo kuisababishia hasara kubwa club hiyo ya New York.

    Hii ndio sehemu  VIP ya club hiyo ya W.i.P ya New York inavyoonekana baada ya timbwili hilo!

Bahati nzuri wakati polisi wa mji huo wanaojulikana kama (NYPD) walipotinga maeneo hayo wasanii hao walikuwa washasepa na hivyo hakuna kati yao aliyekamatwa ingawa uchunguzi wa swala hilo zima umeshaanza na unaendelea.

Habari kwa hisani ya Allhiphop.com!

Post a Comment

 
Top