Menu
 

Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Majanga ya moto yamezidi kuuandama Mkoa wa Mbeya, hususani katika masoko yaliyopo katika wilaya zake mkoani hapa.

Tukio moja la moto mkubwa limetokea Mei 30 mwaka huu majira ya saa 2 kamili usiku katika Kijiji cha Muvwa, Wilaya ya Mbeya Vijijini, ambapo umeteketeza vibanda 10 katika soko la kijiji hicho.

Afisa mtendaji wa kijiji hicho Bwana Kassimu Mpenzi amesema kuwa aligundua kuwepo kwa janga hilo la moto huo ambapo chanzo chake hakikuweza kujulikana.

Aidha thamani ya mali zilizoteketea katika vibanda hivyo haijafahamika mara moja.

Naye, Kamanda wa Polisi mkoani hapa Advocate Nyombi, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba jeshi lake linafanya uchunguzi kuhusiana na tukio hilo.

Mpaka sasa masoko yaliyoteketea kwa moto mkoani hapa na kuleta hasara kubwa ni pamoja na Soko la Mwanjelwa,Viwandani,Sido,Forest,Tunduma,Uyole,Mbeya Vijijini na Black.(Tunduma).

Hata hivyo kutokana na kukua kwa kasi kwa wakazi mkoani hapa bado,taasisi zinazohusika kukabiliana na majanga bado hazijaboreshwa ili kudhibiti matukio ya moto mkoani.

Post a Comment

 
Top